ILI Kufikia uchumi wa kati katika sekta ya Viwanda, mahitaji ya
wakulima, wavuvi na wafugaji hayawezi kutekelezwa kwa bajeti ya serikali
pekee bali wadau wakubwa wajitokeze kuwekeza.
Hayo yamesemwa wakati wa Mkutano wa wadau katika Kuongeza tija kwenye sekta ya kilimo na mifugo kwa maendeleo ya Viwanda.
Mkutano
huo uliodhaminiwa na Benki ya Biashara ya NBC, umeweza kuhudhuriwa na
Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa, Waziri wa Ufugaji na
Uvuvi Luhaga Mpina na Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe.
Benki
ya NBC imesema kuwa itaendelea kushirikiana na kuwasaidia wakulima hasa
katika kuwapatia mbinu mbalimbali za kuboresha , mazao na mbegu zao
kwa lengo la kuhimarisha sekta hiyo.
Mkuu
wa Kitendo cha Wafanyabiashara wadogo na wa kati benki ya NBC, Evance
Luhimbo amesema benki hiyo imekuwa mbele kuwasaidia wakulima wadogo, wa
kati na wakubwa.
Amesema
mikakati yao ya mbeleni kwenye kilimo ni kuhakikisha wanaisaidia sekta
hiyo kwa asilimia kubwa na kwa kuanzia wameaandaa nyaraka inayoelezea ni
kwa jinsi gani mtu anaweza kumsaidia mkulima katika mazao yake na mtaji
wake.
"Tunaowataalamu
wengi ambao tunaendelea kuwatumia kuwasaidia wakulima lakini NBC
tunashirikiana na PASS ambao kazi yao kubwa kuwawekea ulinzi na usalama
wa mazao wakulima," amesema
Aidha,
Bashe amesema kuwa katika sekta ya Kilimo kumekuwa na changamoto kubwa
ya bajeti, kwani haiwezi kutosheleza kwenye kuleta maendeleo ya kilimo
na kufikia malengo yaliyowekwa na serikali.
Amesema,
amewataka mabenki wasitoe mikopo mikubwa sana kwa wakulima kwani
wamekuwa wanawakopesha sawa na wafanyabiashara wengine jambo
linalopelekea wakulima hao kushindwa kulipa kwa wakati.
Waziri
wa Viwanda Bashungwa, amesema katika mwaka 2014-2019 wameingiza chakula
tani Trilion 1.3 jambo ambalo serikali kwa sasa linaangalia namna ya
kuhakikisha uingizaji wa chakula toka nje kinapungua.
Pia,
serikali imeweka mkakati katika kukuza sekta ya viwanda kutoka asilimia
25 hadi 35 katika uzalishaji na kupunguza uingizwaji wa chakula kutoka
nje ya nchi.
Naye Waziri
Mpina ameeleza kuwa kuna fursa kubwa sana katika sekta ya mifugo na
uvuvi ila haijaelekezwa, mvuvi anapata hasara kutokana na kukosa mahali
pa kuanika au kukausha na huu ndiyo wakati wa wajasiriamali kuwekeza.
Waziri wa Ufugaji na Uvuvi akikata utepe kuashiria kuzindua kitabu chenye muongozo wa sekta ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi wakati wa Mkutano wa wadau katika Kuongeza tija kwenye sekta ya kilimo na mifugo kwa maendeleo ya Viwanda wa siku mbili Feb 27-28 unaofanyika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere JNICC na kudhaminiwa na Benki ya Biashara ya Taifa NBC.
Waziri wa Viwanda na Biashara
Innocent Bashungwa (wa tatu kushoto) Waziri wa Ufugaji na Uvuvi Luhaga
Mpina ( wa tatu kulia) na Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe
(katikati) sambamba na Viongozi wa Bodi ya maendeleo ya Kilimo
wakionesha kitabu kilichozinduliwa chenye muongozo wa kuleta tija ya
maendekeo katika sekta ya kilimo na mifugo kwa maendeleo ya
Viwanda. Mkutano huo wa siku mbili Feb 27-28 unafanyika Ukumbi wa
Kimataifa wa Mwalimu Nyerere JNICC na kudhaminiwa na Benki ya Biashara
ya Taifa NBC.
Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe akichangia
mada wakati wa Mkutano wa wadau katika Kuongeza tija kwenye sekta ya
kilimo na mifugo kwa maendeleo ya Viwanda wa siku mbili Feb 27-28
unaofanyika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere JNICC na kudhaminiwa
na Benki ya Biashara ya Taifa NBC.
Mkuu wa Kitendo cha Wafanyabiashara wadogo na wa kati benki ya NBC, Evance Luhimbo akizungumza na
waandishi wa habari na kuelezea mikakati ya benki hiyo katika kuendelea
kuwasaidia wakulima katika uzalishaji bora, Hayo ameyasema wakati wa
Mkutano wa wadau katika Kuongeza tija kwenye sekta ya kilimo na mifugo
kwa maendeleo ya Viwanda wa siku mbili Feb 27-28 unaofanyika Ukumbi wa
Kimataifa wa Mwalimu Nyerere JNICC na kudhaminiwa na Benki ya Biashara
ya Taifa NBC.
Waziri wa Ufugaji na Uvuvi Luhaga Mpina akichangia mada wakati wa
Mkutano wa wadau katika Kuongeza tija kwenye sekta ya kilimo na mifugo
kwa maendeleo ya Viwanda wa siku mbili Feb 27-28 unaofanyika Ukumbi wa
Kimataifa wa Mwalimu Nyerere JNICC na kudhaminiwa na Benki ya Biashara
ya Taifa NBC.
Wadau mbalimbali wa maendeleo wakiendelea kusikiliza Mkutano wa wadau
katika Kuongeza tija kwenye sekta ya kilimo na mifugo kwa maendeleo ya
Viwanda wa siku mbili Feb 27-28 unaofanyika Ukumbi wa Kimataifa wa
Mwalimu Nyerere JNICC na kudhaminiwa na Benki ya Biashara ya Taifa NBC.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...