Na Woinde Shizza, Arusha

TAHARUKI kubwa imeibuka kwa wananchi wa Kijiji cha Ngiresi kilichopo kwenye Kata ya Sokoni 2 katika Halmashauri ya Arusha baada kuzaliwa ng'ombe mwenye vichwa viwili ,midomo miwili na macho matatu .
Kuzaliwa kwa ng'ombe huyo katika eneo hilo kumeibua maswali mengi yasiyo na majibu kwa wananchi hao huku wengi wao wakionekana kushangaa.

Akizungumzia tukio hilo, Mmiliki wa ng'ombe huyo Eliakimu Mungasi ameiambia Michuzi Globu ya jamii kwamba wakati anapewa taarifa ya kuzaliwa kwa ng'ombe huyo alipata mshutuko mkubwa kwani haijawahi kutokea katika maisha yake na kwamba ng'ombe huyo amezaliwa Februari 3 mwaka huu na hasi sasa ametimiza siku 23.

Amesema huu ni uzao wa tano wa ng'ombe aliyezaa ndama huyo ambaye amewashangaza wengi Wa tano ngombe huyo imzaa ndama huyo na kwamba huko nyuma ng'ombe wote walizaliwa walikuwa salama na hawana tatizo lolote.

"Watu wanaongea mengi, wengine wanasema ni mambo ya ushirikina kwa maana ya uchawi, wengine wanasema ni laana lakini mimi sijali, nachojua ni mpango wa Mungu na tutaendelea kumtunza,"amesema Mungasi

Kwa upande wake Elizabeth Mungasi ambaye ni mke wa mfugaji huyo amesema yeye ndio alikuwepo wakati ndama huyo alipokuwa akizaliwa na alishutushwa baada ya kuona mnyama wa aina yake na anatofauti kubwa na ng'ombe wengine.

" Kwani ukizaa mtoto kilema unaweza kumuua, hivyo mimi kama mama nitamlea na nitakaa nae hadi pale ndama huyu atakapo kufa.Tulishamuita daktari akaja akamuona akatuambia hana jinsi ya kutisaidia ,kwa hiyo tukae nae hadi atakapokufa, ndama huyu hawezi kula kitu tunachofanya ni kumkamulia maziwa na kumnyeshwa"alisema Elizabeth 

Wakati huo huo Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi Halmashaur ya Arusha Arusha Charles Ngiroriti amesema hali hiyo ni kawaida kutokea kwa wanyama.Katika utungaji wa kiumbe inaweza ikatokea cell zikagawanyika ,kama vile zilitaka kutengeneza viumbe viwili.

Ameongeza lakini zikishindwa kigawanyika na kufika mwisho ndio anatokea kiumbe wa aina hiyo na kwamba hali hiyo haiuhusiani na imani za kishirikina, hivyo watu waache kuzusha maneno.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...