Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa
 

Na  Mwandishi Wetu, Michuzi Globu ya jamii

MKAZI wa Mbagala jijini Dar es Salaam Ramadhan Rashid maarufu kwa jina la Asney Mjeuri anayetuhumiwa kwa ujambazi sugu ameuawa wakati akitaka kuwakimbia askari Polisi.

Akizungumza leo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amesema kuwa mtuhumiwa huyo wa ujambazi sugu alikamatwa Februari 24 ,2020 saa saba usiku maeneo ya Sabasaba Mbagala Kizuiani jijini.

Mambosasa amefafanua kwamba  kikosi kazi cha kupambana na majambazi klifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo mwenye umri wa miaka 20  ambaye ni mkazi wa Mbagala na wakati mahojiano alikiri kujihusisha na tuhuma mbalimbali za ujambazi maeneo ya Toangoma, Mbagala na Mkuranga.

"Ndipo alikubali kwenda kuwaonesha askari alipoficha silaha na watuhumiwa anaoshirikiana nao na walipofika eneo hilo alianza kukimbia huku akipiga kelele na askari walifyatua risasi tatu hewani kumuamuru asimame lakini mtuhumiwa huyo aliendelea kukimbia na ndipo alipopigwa risasi mgongoni na kufariki dunia papo hapo,"amesema Kamanda Mambosasa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...