Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii
RAIA wa wawili wa China wanaoishi Mkoa Iringa wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shitaka la kutoa rushwa ya Sh. Milioni 11.5 kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)Dk. Edwin Mhede.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa na Wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (TAKUKURU ) Mwakatobe Mshana imewataja washtakiwa hao kuwa ni Heng Rongnan (50) na Ou Ya (47) wote wakazi wa Kinyambo  Mafinga C Iringa.
Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi imedaiwa Februari 24, 2020  jijini Dar es Salaam washitakiwa hao wakiwa katika ofisi za Makao Makuu ya TRA zilizopo ndani ya Wilaya ya Ilala, walitoa rushwa ya Dola za Marekani  5000 sawa na Sh.Milioni 11.5 kwa Kamishna Mkuu wa TRA Dk. Edwin Mhede kwa lengo la kumshwawishi ili aisaidie kwa kampuni yao kutolipa kodi ya Sh. Bilioni 1.3 kiasi ambacho kilipaswa kulipwa kwa TRA.


Washitakiwa hao wamekiri kutenda kosa hilo na Hakimu Shaidi amesema kufuatia washitakiwa kukiri kosa hilo, kesi hiyo utakuja kesho Februari 26 kwa ajili ya kuwasomea maelezo ya awali upande wa mashitaka umetakiwa kumleta mkalimani kwa ajili ya mshitakiwa wa kwanza ambaye hajui kingereza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...