RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizindua Kitabu cha Sheria Zanzibar wakati wa hafla hiyo ya Maadhimisho ya Siku ya Sheria Zanzibar , (kulia kwa Rais) Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu.(Picha na Ikulu).
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akionesha Kitabu cha Sheria baada kukizindua leo katika Maadhimisho ya Siku ya Sheria Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu).
MWANASHERIA Mkuu Zanzibar Mhe.Said Hassan Said, akizungumza wakati wa hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Sheria Zanzibar iliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
WAZIRI wa Sheria na Katiba Zanzibar Mhe Khamis Juma Mwalim akizungumza wakati wa hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Sheria Zanzibar iliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu).
MKURUGENZI Iwa Mashtaka Zanzibar.Mhe Ibrahim Mzee akizungumza wakati wa hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Sheria Zanzibar iliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu) JAJI Mkuu wa Zanzibar Mhe.Omar Othman Makungu akizungumza wakati wa hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Sheria Zanzibar katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdul Wakili Kikwajuni Zanzibar.(Picha na Ikulu).



************************

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amewataka wananchi kuheshimu kazi, majukumu na maamuzi ya Tume za Uchaguzi nchini, kwa kuzingatia kuwa taasisi hizo zimeundwa kwa mujibu sheria na Katiba za nchi.

Dk. Shein amesema hayo katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdul wakil Kikwajuni mjini hapa katika kilelecha maadhimisho ya siku ya sheria Zanzibar.

Alisema kila mwananchi ana wajibu wa kuhakikisha anaheshimu kazi za vyombo hivyo katika uendeshajina utoaji wa maamuzi katika masuala yote yanayohusu uchaguzi wa Zanzibar na ule wa Jamuhuri yaMuungano wa Tanzania.

Alisema wananchi wana wajibu wa kuejiepusha na vitendo vyote vinavyokwenda kinyume na sheria nakanuni zilizowekwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) pamoja na ile ya Jamuhuri ya Muungano waTanzania (NEC).

Alisema ni vyema kuhakikisha kwamba kila mwenye sifa na haki ya kushiriki katika uchaguzi huo, anafanya hivyo kwa kuelewa kuwa huo ni msingi muhimu wa kudumisha utawala bora na Demokrasia.

Aidha, alizitaka taasisi zinazoshughulikia masuala ya uchaguzi pamoja na usalama wa wananchi kufahamu wajibu walionao na kutekeleza majukumu yao ipasavyo, akibainisha umuhimu wa usalama wa nchi kuwa ndio lengo la Serikali. “Ni vyema ikafahamika kuwa suala la kuendeleza demokrasia na kudumisha hali ya usalama na amaniwakati wote ni wajibu wetu wa kikatiba”, alisema.

Alisema Zanzibar ina nafasi ya kujifunza njia bora katika kuendesha kampeni za uchaguzi kwa kuzingatia hoja, ajenda na mambo muhimu ya maendeleo ya jamii na nchi, kama ilivyobainishwa katika Ilani za Uchaguzi badala ya kutumia mwanya huo kufanya kampeni zenye kuleta mifarakano, chuki na uhasama.

Rais Dk. Shein alisema kuna umuhimu wa kuhakikisha kampeni za uchaguzi haziwagawi watu kutokanana rangi zao, makabila yao, dini au miji na vijiji walivyotoka. Akigusi kauli mbiu ya maadhimisho hayo isemayo “Dumisha utawala wa sheria na Demokrasia katika
uchaguzi mkuu 2020”, Dk. Shein alisema suala la kuendeleza Demokrasia na kudumisha hali ya
usalama na amani wakati wote ni wajibu wa kikatiba.

Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetunga sheria ya uchaguzi namba 4 ya 2018, ikiwa ni juhudi za kukuza na kudunisha demokrasia na utawala bora pamoja na kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru nawa haki.

Alisema sheria zimebainisha taratibu zinazopaswa kuchukuliwa pale wananchi wasiporidhika na hatuazilizochukuliwa na moja ya taasisi zinazoshughulikia mchakato wa uchaguzi.
“Iwapo mtu hukuridhika na uamuzi wa Tume ya Uchaguzi anaweza kupeleka shauri lake mahakamani kwa uamuzi”, alisema. Alieleza kuwa uamuzi wowote utakaokwenda kinyume na taratibu zilizowekwa na sheria, zitasababisha zogo na kuanzisha fujo na hivyo kuwa chanzo cha watu kugombana na hatimae kuingiana maungoni.

Alisema Serikali haitasita kuchukulia hatua za kisheria dhidi ya watu wote watakaobainika kuhusika namatukio ya aina hiyo.Alisema kila nchi Duniani ina mfumo wake wa utawala na demokrasia, sambamba na taratibu za kuendesha uchaguzi, ikiwemo namna ya kuwapata viongozi wa kushika nyadhifa tofauti Serikalini. 

“Watanzania tuna mfumo wa Demokrasia unaokidhi hali ya usalama na mazingira yetu na ndio maana sio sahihi na sio halali, si haki na haifai kwa Taifa jengine kuingilia mfumo na taratibu halali za uchaguzi wa nchi yetu zilizowekwa na Tume ya Uchaguzi”, alisema.

Aidha aliwataka viongozi wa vyama vya siasa kuzingatia jukumu kubwa la kuwatumikia na kuwasimamia wanachama na wafuasi wao kwa kuzingatia misingi ya demokrasia na utawala bora. “Si vyema chama cha siasa kushutumu kukosekana kwa misingi ya demokrasia katika chama kingine na taasisi nyengine wakati hali hiyo ni mbaya zaidi ndani ya chama kinacholalamika”, alisema.

Dk. Shein alibainisha kuwa demokrasia ya kweli inahitajika ndani ya uongozi wa vyama vya siasa kwa kuweka misingi bora ya kuendesha chaguzi za viongozi, kutoa fursa za uongozi kwa watu wenye uwezo pamoja na kujiepusha na hatua za kung’ang’ania madaraka.

Alisema wakati Taifa likijiandaa na uchaguzi mkuu ujao, ana imani kubwa na vyombo vya sheri na kusisitiza umuhimu wa kutekeleza vyema majukumu yao kwa uadilifu na haki. Alisema Serikali itaendelea kuhakikisha hali ya amani na utulivu nchini inaendelea kudumu, na kuwakumbusha wananchi jukumu la kuimarisha utawala wa sheria pamoja na kulinda usalama.

Akigusia juu ya uhuru wa mahakama, Dk. Shein alisema katika kipindi chote akiwa madarakani hajawahi wala kuweka azma ya kuingilia uhuru wa chombo hicho, kwa kutambua kuwa ndio nguzo na mhimili wa utawala usiopaswa kuingiliwa.

Alitoa shukurani kwa watendaji wote wa Mahakama pamoja na wale waliochangia na kushiriki katikautayarishaji wa toleo la nane la Kitabu cha “Zanzibar Yearbook of Law”, akibainisha matumaini yake kuwakitabu hicho kimetayarishwa baada ya kufanyika utafiti wa kutosha.

Aidha, aliwapongeza watendaji hao kwa ubunifu wao wa kuanzisha programu maalum ya kwenda kwawananchi, hususan walioko vijijini kwa ajili ya kuwapatia elimu ya kufahamu haki zao za kikatiba nakisheria.

Mapema, Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu alisema sherehe hizo, alisema kwa vipindi
tofauti nUchaguzi wa Zanzibar umekuwa na ushindani mkubwa wa kisiasa, hivyo akasisistiza umuhimuwa jamii kuendelea kulinda amani iliopo.

Alisema mfumo wa Demokrasia ya vyma vingi kamwe haupaswi kuwa sababu za kuvuruga amani iliopo,akibainisha matukio kadhaa yaliojitokeza katika chaguzi zilizopita kutokana na wananchi kutotii sheria.

Makungu alitoa ushauri kwa kuwataka wanasheria na mawakili wa kujitegemea kupelekea mapendekezoyao Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili kusikilizwa kwa kuzingatia kuwa Serikali hii ni sikivu, kablaya kuwasilisha mahakamani.

Alisema Idara ya Mahakama imejipanga kuleta mabadiliko makubwa ya kiutendaji katika miaka mitano ijayo katika suala zima la utoaji wa huduma. Nae, Waziri wa Katiba na sheria khamis Juma Mwalimu, alitowa wito kwa wananchi kuendelea kuheshimu na kutii sheria za nchi, kwa kuzingatia kuwa hakuna mtu yeyote alie juu ya sheria.

Alisema Wizara hiyo itaendelea na jukumu la kusimamia Utawala wa sheria na upatikanaji wa haki kwawananchi wote. Aidha, Mwanasheria Mkuu wa serikali ya Zanzibar Said Hassan Said, alisema wakati wa kushereherekeasiku ya sheria Zanzibar, kuwa hiyo ni fursa ya kuwakumbusha wananchi juu ya haki waliyonayo yakupiga kura kwa kuzingatia misingi ya utawala bora na utawala wa sheria.

Alisema dhana ya Utawala bora na utawala wa sheria ni nguzo muhimu ya kuifanya Demokrasia ishamirina kuleta ustawi wa jamii pamoja na maendeleo yao. Alisema kila Mzanaibari anayo haki na uhuru wa kushiriki katika mchakato wa uchaguzi ili kufikia maamuzi yatakayoleta hatma njema ya maisha yake na Taifa na kusisitiza wajibu wa kila mwananchi mwenye sifa kujiandikisha.

Alitoa wito kwa wanancho wote kutumia fursa ya kuchagua viongozi kwa kuelewa kuwa fursa hiyo
hupatikana kila baada ya miaka mitano. Vile vile, Mkurugenzi wa Mashtaka Ibrahim Mzee Ibrahim, alisema Ofisi hiyo ina wajibu wa kuwachukulia hatua za kisheria watu wote na taasisi zitakazotenda makosa ya uchaguzi, hivyo akasisitiza haja ya taasisi zinazoshughulikia mchakato wa uchaguzi kusimamia vyema majukumu yao.

Katika hafla hiyo iliyohudhuria na Viongozi mbali mbali wa Serikali na wadau wa sekta ya Sheria, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Moahmed Shein, alizindua kitabu cha ‘Zanzibar YearBook of Law’ pamoja na kupokea zawadi maalum iliyoandaliwa na Uongozi wa Idara ya Mahakama Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...