Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ( wa tatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja  na Watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) mara baada ya kufunga mafunzo ya siku sita ya matumizi ya mifumo ya TEHAMA katika utendaji kazi kwa  Watendaji wa TRA wa Mikoa ya Katavi, Kigoma na Tabora wanaohusika na ukusanyaji wa mapato.
 Baadhi ya Watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) wakiwa katika siku ya mwisho ya  mafunzo ya siku sita  ya matumizi ya mifumo ya TEHAMA katika kuongeza utendaji kazi kwa  Watendaji wa TRA wa Mikoa ya Katavi, Kigoma na Tabora wanaohusika na ukusanyaji wa mapato.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akifunga  mafunzo ya siku sita ya matumizi ya mifumo ya TEHAMA katika utendaji kazi kwa  Watendaji wa TRA wa Mikoa ya Katavi, Kigoma na Tabora wanaohusika na ukusanyaji wa mapato.

Na Tiganya Vincent,Tabora
WATUMISHI wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wametakiwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kujenga mazingira rafiki kwa mlipa kodi ili aweze kutumia mifumo hiyo katika ulipaji kodi na hivyo kuongeza mapato ya Serikali.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akifunga mafunzo ya siku sita ya matumizi ya mifumo ya TEHAMA katika utendaji kazi kwa  Watendaji wa TRA wa Mikoa ya Katavi, Kigoma na Tabora wanaohusika na ukusanyaji wa mapato.

Alisema ni vema wakatumia elimu waliyopata kuboresha utoaji wa huduma ambap watamfanya  Mlipa kodi aweze kutumia muda mfupi na gharama nafuu katika ulipaji kodi jambo ambalo litasaidia kuongeza mapato ya Serikali.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka Wafanyakazi hao wa TRA kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili wajue wajibu wao katika kulipa kodi kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

Naye Meneja wa Mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Lazaro Swai alisema lengo la mafunzo hayo ilikuwa ni  kuwaongezea ujuzi watumishi ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi na hivyo kuongeza mapato ya Serikali.

Alisema kuwa elimu waliyopata itawasaidia kuwawezesha walipa kodi kuweza kulipa Kodi katika mazingira jirani ikiwemo Ofisi kwao au kwa Wakala badala ya kusafiri hadi TRA na kutumia muda na gharama za usafiri.

Swai alisema Mifumo ikitumika vizuri itasaidia kuongeza ukusanyaji wa mapato ya Serikali na hivyo kuwa na fedha nyingi za kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi.

Kwa upande wa Meneja wa TRA Mkoa wa Tabora Thoams Masese alisema mafunzo yaliyotolewa yatawasaidia watumishi wa TRA katika kuwasaidia walipa kodi ili waweze kulipa katika mazingira ambayo wataona ni rahisi kwao na kuwapunguzia usumbufu na hivyo kuwezesha kuongeza makusanyo ya Serikali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...