Na Zainab Nyamka, Michuzi TV.

Kocha wa timu ya Sahare All Stars Kessy Abdalla amesema wamejipanga kucheza na timu yoyote watakayopangiwa nayo kwenye mchezo wa robo fainali ya Kombe la Azam ASFC.

Hayo ameyasema baada ya kumalizika kwa mchezo wa hatua ya 16 bora baada ya kuibuka na ushindi wa goli 5-2 dhidi ya Panama Fc ya Jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo umechezwa leo katika Uwanja wa Uhuru ambapo Sahare All Stars waliweza kuibuka na ushindi huo mnono.

Kocha Abdalla amesema kuwa wao wanaamini kuwa timu yoyote watakayopangiwa nayo hawataidharau bali watapambana kuhakikisha wanafanya vizuri ili kufika mbali zaidi kwenye kombe la Shirikisho.

"Sisi tupo vizuri, tuko tayari kucheza na timu yoyote ile tutakayopangiwa nao kwenye hatua ya nane bora, tutaingia kwa tahadhari ili tuweze kuibuka na ushindi na kufika hadi fainali,"amesema Abdalla

Aidha, ameelezea kuwa nidhamu ya mchezo ndio imepelekea wao kuwaondoa Mtibwa hatua ya 32 bora na hata leo kwenye hatua ya 16 bora dhidi ya Panama.

Naye Mjumbe ww Kamati ya Utendaji wa Sahare All Stars, Mussa Adinani 'Kashasha' amesema kuwa wanaamini ushindani katika hatua inayofuata utakuwa ni mkubwa sana ila wamejipanga kuweza kushinda kwenye mchezo huo

Amesema, wameshinda ushindi wa kishindo kwa kumfunga Panama goli 5 na hio ni salamu kwa timu zingine zitakazokutana kwenye kombe la shirikisho.

Akizungumzia maandalizi ya ligi daraja la Kwanza (FDL) Kashasha amesema wanafahamu wapo nafasi ya saba kwenye kundi A ila katika mechi zilizosalia ili kusalia na kujipanga kwa msimu ujao.

Pia, amewatahadharisha wapinzano kuwa hawataruhusu kupoteza mchezo wowote kwa sasa ambapo wanaelekea kanda ya ziwa kucheza mechi nne mfululizo.

Magoli ya Sahara yamefungwa na Hussein Zola,Kassim Tiote  akifunga , Ally Salim  na issa Ubaya.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...