Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima akiangalia hatua za uchakataji wa dhahabu kwa wachimbaji wadogo kijiji cha Sambaru wilayani Ikungi mkoani Singida ambapo aliwapa elimu kuhusu namna ya kujikinga na wanapotumia kemikali ya zebakia ambayo ina madhara kwa afya na mazingira. Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima akizungumza na wachimbaji wadogo katika mgodi mdogo ulipo kijiji cha Sambaru wilayani Manyoni mkoani Singida ambapo aliwaelimusha kuhusu madhara ya kutumia zebaki. Kulia ni Kaimu Meneja wa Ofisi ya Madini Mkoa wa Singida, Chone malebo. Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima akipewa maelezo kuhusu namna hatua za uchimbaji hadi uchakataji wa dhahabu unavyofanyika wakati akiwa katika ziara eneo la wachimbaji wadogo kijiji cha Sambaru wilayani Ikungi mkoani Singida. Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima  akielekea kukagua shughuli wanazofanya wachimbaji wadogo pamoja na namna wanavyotunza mazingira katika machimbo ya kijiji cha Sambaru. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Edward Mpogoro. Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima akiangalia namna ambavyo uchenjuaji wa dhahabu kwa kutumia zebaki katika mgodi mdogo uliopo kijiji cha Sambaru wilayani Manyoni mkoani Singida ambao unafanyika bila kutumia vifaa maalumu vya kujikinga mikono jambo ambalo linaleta madhara kwa afya na mazingira. Sehemu ya wachimbaji wadogo kijiji cha Sambaru wilayani Ikungi mkoani Singida alipofanya ziara ya kukagua shughuli za wachimbaji wadogo wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima (hayupo pichani) wakati akizungumza nao kuhusu madhara ya zebaki kwa afya na mazingira. Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima akiangalia namna ambavyo uchenjuaji wa dhahabu kwa kutumia zebaki katika mgodi mdogo uliopo kijiji cha Sambaru wilayani Manyoni mkoani Singida. Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima akizungumza na mwananchi aliyemkuta akifanya shughuli za kuponda mawe katika eneo la wachimbaji wadogo kijiji cha Sambaru wilayani Ikungi mkoani Singida alipofanya ziara ya kukagua shughuli za wachimbaji wadogo.

…………………………………………………..

Na Robert Hokororo, Singida

Wakati Serikali inaendelea kuweka utaratibu wa kupata mbadala wa matumizi ya zebaki kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu imeshauri watumie vifaavinavyowakinga wakati wakifanya shughuli hizo.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira) Mhe. Mussa Sima wakati akizungumza na wachimbaji wadogo kwanyakati tofauti katika vijiji vya Sambaru wilayani Ikungi na Londoni wilayaniManyoni mkoani Singida.

Sima alisema kuwa Serikali inaendelea na kuwapa elimu wachimbaji hao katika maeneo mbalimbali nchini ili waweze kuepuka madhara ya kiafya yanayotokana na kemikali hiyo.

“Tanzania tuliridhia Mkataba wa Minamata mwaka jana unaotaka kupunguza ama kuondoa kabisa matumizi ya zebaki kwa ninyi wachimbaji ili kuwaepusha madhara ya kiafya na kimazingira katika maeneo yenu,” alisema naibu waziri.

Akiwa katika ziara hiyo ambapo alitembela kuona shughuli za uchimbaji na
kukagua namna wanavyotunza mazingira, Sima alisema kuwa jukumu la Serikali ni kutoa elimu juu ya madhara ya zebaki ili kulinda afya za wachimbaji wadogo.

“Niwaahidi tu tutashirikiana na Ofisi ya Madini ili muweze kupata vifaa maalumu vya kujikinga wakati wa kuchenjua badala ya mikono, tutawaletea gloves mvae mikononi na musk wakati tunachoma ili kufunika pua kwani kemikali hii ina madhara kiafya,” alisema.

Aidha, Naibu waziri aliwataka wachimbaji hao kuacha kukata miti wakati washughuli za uchimbaji wa dhahabu na badala yake wawe na utamaduni wakutumia njia mbadala kama ambavyo wanavyoelekezwa na mamlaka
zinazohusika.Aliongeza kuwa jukumu la Ofisi ya Makamu wa Rais na Serikali kwa ujumla nikuhakikisha nchi inakabiliana na changamoto ya mabadilkko ya tabianchi na hivyo kuleta athari.

Alisema tunapoendelea kuchoma na kukata miti ovyo, kulima kholela na
kuchimba mashimo ovyo kwa ajili ya madini ni mambo yanayosababisha mvua isije kwa wakati pamoja na jua kuwa kali kuliko kawaida.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...