Na Said Mwishehe, Michuzi TV
TIMU ya soka ya Simba ya jijini Dar es Salaam imefanikiwa kuingia hatua robo faina ya michuano ya Azam Sports Federation CUP baada ya kuibuka na ushindi kwenye mchezo wao wa leo dhidi ya Stand United.

Mchezo kati ya timu ya Simba na Stand United umepigwa katika dimba la Kambarage Shinyanga na hadi mpira huo unamaliza timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 na hivyo kuingia hatua ya matuta.
Hatua hiyo ya matuta iliiwezesha Simba kushinda penalt 3 -2 ambapo kwa upande wa Simba walioshinda penalt hizo Hassan Dilunga, Chota Chama na Deo Kanda na waliokosa ni Ibrahim Ajibu na Medie Kagere.Kwa upande wa Stand United waliokosa penalt walikuwa wachezaji watatu akiwemo Miraji Salehe na Maulid Fadhil

Kabla ya hatua ya kupigwa penalt, mchezo huo ulikuwa na raha ya aina yake kutokana na wachezaji wa timu zote mbili kila mmoja kucheza mpira wwenye ufundi mkubwa kiasia cha kuleta buradani kwa waliokuwa wanafuatilia mechi hiyo.

Simba walipata bao la kwanza kupitia mkwaju wa penalt lililofungwa na Hassan Dilunga katika dakika ya 60.Hata hivyo Stand United walipata bao la kusawazisha kupitia kwa mshambualiaji wake Miraji Salehe.Hivyo mchezo ukamalizika kwa sare ya 1-1.

Timu nyingine ambazo zimeingia hatua ya robo katika fainali hiyo ni timu Namungo FC, Ndanda FC pamoja na Sahare All Stars. Michezo mingine inatarajia kufanyika kesho ukiwemo mchezo wa timu ya soka ya Yanga dhidi Gwambina pamoja na Ihefu FC dhidi ya Azam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...