Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. William Paul Ntinika akiwa katika picha ya pamoja na Msafara wa kijinsia wa kutokomeza ukatili wa kijinsia mara baada ya kuwasili mkoani hapo.
 Mkuu wa Wilaya ya Mbeya,William Paul Ntinika akizungumza na vikundi vya wanawake wajisiriamali walijitokeza kuupokea msafara wa kijinsia wa kutokomeza ukatili wa kijinsia ulipowasili mkoani hapo.
 Mkuu wa Wilaya ya Mbeya William Paul Ntinika pamoja na wasanii Shetta, G Nako na wawakilishi wa Msafara wa kijinsia wa kutokomeza Ukatili wa kijinsia wakicheza wimbo maalum wa Kampeni ya Twende Pamoja.

Na Mwandishi Wetu Mbeya
MKUU wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chamila amesema vitendo vya ukatili wa kijinsia havitokei kwa wanawake pekee bali hata wanaume wanapigwa na kunyanyaswa na wanawake.

Hayo yamesemwa kwa niaba yake leo mkoani humo na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. William Paul Ntinika alipokuwa akiupokea msafara wa kijinsia wa kutokomeza ukatili wa kijinsia ulipowasili mkoani hapo.

Mhe. Ntinika amesema kuwa jamii imekuwa iikiweka nguvu katika kuwatetea wanawake kwa kuwa wamekuwa wakitoa taarifa ya kufanyiwa vitendo vya ukatili kwa wanawake hivyo nguvu pia inahitajika ya kutoa elimu kwa wanaume ili waweze kutoa taarifa ya vitendo hivyo.

Ameongeza kuwa Serikali inaendelea katika kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa dhidi ya wanawake na watoto kwa kuanzisha mipango na Sera mbalimbali zinazosaidia kutoa elimu kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo katika mapambano ya vitendo vya ukatili wa kijinsia.

"Sisi mkoa wa Mbeya tuko vizuri tunapambana na vitendo vya ukatili juzi tu tulipata taarifa kutoka kwa mtoto kuwa anafanyiwa vitendo vya ukatili na baba yake na tumeshamchukulia hatua za kisheria"alisema

Akizungumzia malengo ya msafara wa kijinsia Mwakilishi wa Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bi. Imelda Kamugisha amesema msafara huo umelenga kutoa elimu kwa jamii kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia katika familia na jamii kwa ujumla.

"Kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani tumekuja na msafara wa kijinsia ili tuweze kutoa elimu kwa wanajamii kuhusu kupambana na vitendo vya ukatili" alisema

Kwa upande wake Balozi wa Kampeni ya Twende Pamoja Nurdin Bilal 'Shetta' amesema suala la mapambano ya ukatili wa kijinsia ni suala la jamii yote katika mapambano hayo hivyo wameungana na Serikali katika kuhakikisha elimu inaifikia jamii ili kuondokana na vitendo hivyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...