Mshauri Mwandamizi, Bw. Shielles Tenaw, (kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Dkt. Pancras Bujulu, (katikati) wakimfuatilia kwa makini mmoja wa wanafunzi wa Fani ya Ufundi Mitambo (Fitter Mechanics), katika Chuo cha VETA Dar es Salaam, akiwaonesha utendaji kazi wa mashine na mitambo mbalimbali walipotembelea Karakana y Ufundi Mitambo, Chuoni hapo.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Omnia Espoo, Sampo Suihko, (kushoto), akifuatilia kwa makini maelezo ya Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Dkt. Pancras Bujulu, (katikati), wakati wa majadiliano na Menejimenti ya VETA kwenye ofisi za VETA Makao Makuu. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala, Bw. Felix Staki.

VETA ilitembelewa na ujumbe wa watu wawili kutoka Taasisi ya Omnia Espoo ya nchini Finland ukiwahusisha Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo, Bw. Sampo Suihko na Mshauri Mwandamizi, Bw. Shielles Tenaw. Waliambatana na Afisa Mwandamizi, Idara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Bi. Fides Lubuva.

Suihko na Tenaw wapo nchini tangu tarehe 7 Februari 2020 wakitembelea Taasisi mbalimbali za Elimu na Mafunzo nchini kwa lengo la kuangalia namna bora ya kuanzisha ushirikiano kati ya Taasisi ya Omnia Espoo na Taasisi za Tanzania katika maeneo mbalimbali ya mafunzo ya ufundi. 

Wanatarajia kuhitimisha ziara yao tarehe 23 Februari 2020 wakiwa wametembelea Baraza la Elimu na Mafunzo ya Ufundi (NACTE); Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE); Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia Zanzibar; Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT); Chuo Kikuu cha Dodoma, Wizara mbalimbali na VETA. 

Wakiwa VETA, walifanya mazungumzo na Menejimenti ya Makao Makuu, kisha kutembelea karakana mbalimbali za Vyuo vya VETA Dar es Salaam na VETA Kipawa. Jumatano, tarehe 12 Februari pia walitembelea chuo cha VETA Dodoma. 

Kwa mujibu wa Watendaji hao, maeneo mahsusi yanayolengwa na Taasisi ya Omnia Espoo katika ushirikiano na Tanzania ni pamoja na Kuboresha Ufundishaji; Mafunzo ya Uanagenzi; Mitaala ya Kufundishia Stadi za Uvuvi katika Kina Kirefu (Deep Sea Fishing) na Sekta ya Misitu.

Suala Kuboresha Ufundishaji linazingatia ukweli kuwa Finland imekuwa nchi iliyo katika nafasi ya Juu Duniani kwa Kiwango cha elimu kutokana na Mfumo Mzima wa Ufundishaji. 

Kwa kuzingatia hilo, ushirikiano na Finland katika kuboresha ufundishaji unaweza kusaidia kutoa wahitimu bora na wanaoweza kufanya kazi katika mazingira tofauti tofauti. 

Majadiliano na Menejimenti ya VETA yamehitimishwa kwa makubaliano ya kutumia fursa zilizopo za kimataifa kati ya Tanzania na Finland na kati ya nchi hizi mbili na mashirika na programu mbalimbali za kimataifa kuanzisha ushirikiano rasmi, hususan katika tasnia hii ya ufundi stadi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...