Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV

TASISI ya Basic Internet Foundation (BIF)imesema kwamba limetambua matumizi ya mtandao itakayosaiflla kukuza utangamano wa nchi rafiki.

Hayo yalibainishwa leo jijini Dar es Salaam na Katibu wa Internet Inclusion,Profesa Josef Noll alipokutana na wadau wa nchi nne ikiwemo mwenyeji wao Tanzania kwa lengo la kujadili umuhimu wa matuminzi ya internet hasa katika shule na vijijini.

Josef amesema ili kutambua matumizi ya internet yanayokuwa kwa kasi wakaona umuhimu kuanzia na shule , hospital na jamii.

Amesema kuwa BIF imeweza kuunganisha mtandao katika vitongoji 10 nchini Tanzania na kuongeza kuna tayari ku a shule ambazo nazo zimeunganishiwa mtandao na hivyo kurahihisha mawasiliano ya mtandao kwenye maeneo hayo na lengo ni kuzifikia shule zote nchini.

Ameongeza kwa Chuo cha Ualimu Patandi wamekuwa na huduma ya mtandao kwa zaidi ya miaka miwili huku akieleza wamekuwa wakifanikisha uunganishaji mtandao kwa kushirikiana na Wizara ya Mawasiliano.

Amesema jitihada ambazo zinaendelea nchini Tanzania katika kuongeza huduma ya Intanet karibu na wananchi ndio moja ya sababu ya BIT kuandaa mkutano huo uliojulikana kama Hackathan ambao umekutanisha nchi za Kenya,Zambia,Zimbabwe na mwenyeji Tanzania ,ili kupeana mafunzo jinsi ya matuminzi ya mtandao na mawasiliano.
 Katibu Mkuu wa Taasisi ya Intarnet Inclusion Profesa Josef Noll akifafanua jambo kuhusu matumizi ya intanet nchini Tanzania baada ya kufanyika kwa wadau wa mtandao nchini
Wadau wa masuala ya mtandao wakijadiliana jambo wakati wa mkutano  uliokutanisha wadau mbalimbali

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...