Waziri wa zamani wa Viwanda na Biashara katika serikali ya Awamu ya Tatu Mzee Iddi Mohamed Simba amefariki dunia leo asubuhi katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu, binti yake Sauda Simba amethibitisha.
RATIBA YA MAZISHI
RATIBA YA MAZISHI
Kwa mujibu wa taarifa za kifamilia, mwili wa Marehemu Iddi Mohamed Simba utaoshwa katika msikiti wa Maamur ulioko Upanga jijini Dar es salaam kabla ya kupelekwa nyumbani kwake Mikocheni Plot 109 mnamo saa mbili asubuhi, ambapo ndugu, jamaa, marafiki na majirani watakusanyika kumuombea dua hapo nyumbani.
Itapofika saa 5 asubuhi mwili wa Marehemu utapelekwa msikiti wa Manyema mtaa wa Mafia na Lumumba, Kariakoo, ambapo kutakuwa na dua pia. Kisha baada ya swala ya Ijumaa, itafuatia Swalat Jeneiza kisha mwili utapelekwa Magomeni kwenya makaburi ya Mwinyimkuu kwa mazishi.
Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un
إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ

RIP mzee Simba
ReplyDelete