Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw. Godfrey Nyaisa amesema kwamba matatizo yote katika Mfumo wa usajili kwa njia ya mtandao (ORS) sasa kuwa historia.

Hayo ameyabainisha wakati akijibu hoja za wafanyabiashara wa Mkoa wa Simiyu siku ya jana tarehe 25 Februari, 2020 katika kikao cha mashauriano kati ya serikali na Wafanyabiashara.

Akizungumza katika kikao hicho Bw. Nyaisa amebainisha kwamba, BRELA imechukua hatua za makusudi katika kutatua changamoto katika mfumo wa usajili na punde itabaki kuwa historia.

“Katika kutatua changamoto katika mfumo marekebisho makubwa ya kimfumo yanafanyika na mpaka hivi sasa mfumo unafanya kazi katika hali ya kawaida, pia jitihada zaidi zinaendelea kufanyika ili kuhakikisha kwamba kwa wakati wote wadau wetu wanapata huduma” alibainisha Bw. Nyaisa.

Katika hatua nyingine Bw. Nyaisa ametoa habari njema kwa wadau wa BRELA juu ya Ujio wa kituo cha miito (Call center).

Ambapo ameeleza kwamba kituo hiki kitakua ni msaada mkubwa kwa wadau wote waliombali pale wanapopiga simu waweze kupata msaada wa haraka.

Kwa kutumia mfumo huu, pale wadau wanapopiga simu kwa ajili ya msaada simu hiyo inaenda katika namba iliyo huru kwa wakati huo.

Mkutano huo umefanyika chini ya Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji Mhe. Angellah Kairuki akiambatana na Manaibu Waziri saba kutoka Wizara za Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Fedha na Mipango, Mambo ya Ndani ya Nchi, Madini, Maliasili na Utalii, Mazingira pamoja na Viwanda na Biashara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...