*Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kassim Majaliwa aipongeza TCRA

Na Chalila Kibuda Globu ya Jamii aliyekuwa wilayani Ruangwa

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)Kanda ya Mashariki imetoa elimu ya Mawasiliano katika Shule mbili za Sekondari wilayani Ruangwa  ili   Wanafunzi na walimu wajue namna ya kutumia mawasiliano hayo kwa usalama.

Shule za Sekondari zilizipata elimu ya Mawasiliano wilayani Ruangwa ni  Kassim Majaliwa na Likunja

Akizungumza kwa nyakati tofauti katika Shule hizo Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa (TCRA) Mhandisi Lawi Odiero amesema kuwa Wanafunzi wakiwa na elimu ya utumiaji wa mawasiliano ni mabalozi wazuri wa kuelimisha wengine pamoja na wao wakifikia umri wa kumiliki simu na bidhaa zingine za Mawasiliano watakuwa wanatumia kwa usalama.

"Ninaamini Wanafunzi wetu wakipata elimu ni hakika wataweza kuelimisha wengine utumiaji wa mawasiliano kwa usalama pamoja na wao kuwa kizazi bora wakati wakiwa wametimiza umri wa kumiliki simu kuzingatia matumizi salama ya utumiaji wa simu hizo na huduma mbalimbali za mitandao"amesema Mhandisi Odiero.

Mhandisi Odiero amesema kuwa TCRA ndio wadhibiti wa mawasiliano hivyo wanawajibu wa kuwalinda watumiaji katika matumizi salama ya Mawasiliano.

Aidha amesema kuwa utoaji wa elimu hiyo ni endelevu kutokana na teknolojia ya Mawasiliano kubadilika kila wakati hivyo TCRA lazima iendane na mabadiliko hayo.

Nae Mkuu wa Shule wa Sekondari ya  Kassim Majaliwa ,Mohamed Lukanga  amesema kuwa kwa elimu waliopata wataitumia kuelimisha wengine pamoja na wanafunzi kuwa mabalozi katika jamii wanayoishi.
  
Amesema kuwa TCRA imethubutu katika utoaji wa Elimu ya Mawasiliano katika makundi mbalimbali nia ni kuwa na matumizi salama ya Mawasiliano.

Kwa upande wa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari  Likunja Neema Lugongo  amesema TCRA wamefika wakati mwafaka kutokana wa kuelimisha namna ya kutumia Mawasiliano salama ya simu na mitandao mbalimbali.
 Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Lawi Odiero akizungumza na wanafunzi wa  Shule ya Sekondari Kassim Majaliwa wilayani Ruangwa mkoani Lindi. 
 Mkuu  wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Lawi Odiero akizungumza na wanafunzi na Walimu  wa  Shule ya Sekondari Likunja wilayani Ruangwa mkoani Lindi. 
 Mhandisi Mwandamizi wa Kanda ya Mashariki  wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Christopher John akitoa mada ya haki na wajibu kwa watumiaji wa Mawasiliano Katika Shule ya Sekondari  Kassim Majaliwa   wilayani Ruangwa  mkoani Lindi.
 .Afisa wa Kanda ya Mashariki  wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Annastella Mchomvu akimkabidhi zawadi ya simu mwalimu wa Shule ya Sekondari Likunja Yuda Alfa wakati Kanda hiyo ilipokwenda kutoa elimu katika shule hiyo. 
 Mkuu  wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Lawi Odiero akimkabidh Kitabu cha moongozo wa Mawasiliano Mwalimu Mkuu  wa Shule ya Sekondari Likunja  Neema Lugongo wakati Kanda hiyo ilipokwenda kutoa elimu katika shule hiyo. 
 Mkuu  wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Lawi Odiero  (mwenye miwani)akimkabidh Kitabu cha moongozo wa Mawasiliano Mwalimu Mkuu  wa Shule ya Sekondari Kassim Majaliwa  wilyani  Ruangwa Mohamed Lukanga   wakati Kanda hiyo ilipokwenda kutoa elimu katika shule hiyo.
  Baadhi ya wanafunzi wa  Shule ya Sekondari  Kassim Majaliwa  wilayani a Ruangwa wakipata elimu ya Utumiaji wa Mawasiliano. 
Picha ya pamoja kati ya TCRA ,Walimu na Wanafunzi  wa Shule ya Sekondari Likunja mara baada TCRA kutoa elimu katika shule hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...