Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii

HIVI karibuni Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA )imetoa utabir wake wa Mvua  za masika kwa kipindi cha Machi hadi Mei,2020 ambazo  zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani .

Mvua hizo zinatarajia kunyesha katika maeneo ya Mkoa wa Tanga, Visiwa vya Unguja na Pemba, maeneo mengi ya Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro, Mashariki mwa Mkoa wa Geita pamoja na Mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Simiyu na Mara.

Maeneo ya Mkoa wa Kagera, magharibi mwa Mkoa wa Geita, kaskazini mwa mkoa wa Kigoma, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha kisiwa cha Mafia) pamoja na kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro yanatarajiwa kupata mvua za wastani hadi chini ya wastani.

Huku Mvua za nje ya msimu zinazoendelea kunyesha katika maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka, hususan yaliyopo katika pwani ya kaskazini zinatarajiwakuendelea na kuungana na msimu wa mvua wa masika 2020.

Akizungumzia kuhusiana na athari zinazotarajiwa kutokea kutokana na mvua hizo, Mkurugenzi wa Mamlaka ya hali Hewa Tanzania (TMA ), Dkt. Agnes Kijazi amesema unyeshaji wa mvua hiyo inauwezo wa kuleta athari mbalimbali ikiwemo ya milipuko ya magonjwa na wadudu waharibifu .

Aidha anasema Kwa kuzingatia  matumizi sahihi ya huduma za hali ya hewa kwa kiasi kikubwa nchi inaweza  kupunguza athari za uharibifu wa mazingira hivyo ni vema wananchi wakachukulia umakini utabiri wa hali ya hewa na kuepuka manga mbali mbali yanayoweza kujitokeza kutokana na mvua hizo.

Dkt. Kijazi amesema pia uchimbaji wa madini ufanyike kwa kuzingatia utabiri uliyotolewa kwani ongezeko la maji katika udongo linaweza kusababisha maporomoko ya ardhi hususan katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za wastani hadi juu ya wastani.

"Vipindi vifupi vya mvua kubwa vinaweza kujitokeza hata katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za wastani hadi chini ya wastani,hivyo jamii inashauriwa kuchukua hatua stahiki kupunguza athari zinazoweza kujitokeza,"amesema Dkt.Kijazi

Amesema Maeneo yanayotarajiwa kuwa na mvua za wastani hadi juu ya wastani,zinaweza kufaa kwa uzalishaji wa mazao ikiwa ni pamoja na yale yanayoweza kustawi kwenye unyevunyevu wa udongo uliyopitiliza kama vile mpunga.

Aidha Dkt. Kijazi amesema kwa sasa TMA inavitendea kazi vingi na vya kutosha ambavyo vinasaidia upatikanaji sahihi wa utabiri ambapo mpaka sasa taarifa za utabiri zinazoandaliwa zine ubora na zinaweza kutumika kwa usahibi kwa zaidi ya asilimia 80.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...