Na Karama Kenyunko, Michuzi Globu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Februari 17 mwaka  2020 imeshindwa kuendelea na makubaliano katika kesi a Uhujumu Uchumi inayomkabili  Mwandishi wa Habari Erick Kabendera kwa sababu Hakimu anayesikiliza kesi hiyo amepata udhuru.

Kwa mujibu wa ratiba ya kesi hiyo leo ilitegemewa kuwa ni hatma ya mwisho ya Kabendera kusota rumande tangu alipopandishwa kizimbani Agosti 5,mwaka  2019 baada ya kuingia makubaliano na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP).

Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon  amedai mbele ya Hakimu Mkazi Vicky  Mwaikambo kuwa shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kutajwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Janet Mtega anayesikiliza kesi hiyo hayupo hivyo ameomba kesi hiyo iahirishwe hadi tarehe nyingine.Hakimu Mwaikambo ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 24, 2020 kwa ajili ya kutajwa.

Katika kesi hiyo, Kabendera anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka matatu likiwemo la utakatishaji wa Sh.Mil 173. Inadaiwa kuwa katika kipindi hicho, Kabendera alijihusisha na mtandao wa kihalifu kwa kutoa msaada kwa genge la uhalifu kwa nia ya kujipatia faida.

Inadaiwa kuwa katika kipindi hicho, bila ya sababu alikwepa kodi ya Sh.Mil 173,247,047.02 ambayo ilitakiwa ilipwe Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Pia inadaiwa Kabendera alitakatisha Sh.173,247047.02 huku akijua fedha hizo ni mazalia ya kosa la kujihusisha na genge la uhalifu na ukwepaji kodi.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...