MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imesema Aprili Mosi Mwaka  huu itatoa uamuzi dhidi ya kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Kawe, Halima Mdee kama ana kesi ya kujibu au la.

Uamuzi huo utatolewa na Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba kufuatia upande wa mashtaka uliowakilishwa na wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon kudai mahakamani hapo leo Februari 20, 2020 kuwa wamedunga ushahidinhao.

"Mheshimiwa shauri leo limekuja kwa  kutajwa lakini nimepitia ushahidi uliotolewa na mashahidi watatu wa upande wa mashitaka na nimeona tufunge ushahidi." amesema Wankyo.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba amewapa siku 14 upande wa utetezi kuwasilisha maelezo kama mshitakiwa huyo ana kesi ya kujibu au la na pia alitoa siku 14 kwa upande wa mashitaka kujibu hoja hizo.

Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Aprili Mosi mwaka huu kwa ajili ya kutoa uamuzi kama Mdee ana kesi ya kujibu au la.

Katika kesi hiyo  mashahidi watatu wa upande wa mashitaka wametoa ushahidi akiwamo  Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Urafiki, Mrakibu wa Polisi (SP) Batseba Kasanga.

Katika kesi hiyo, inadaiwa kuwa Julai 3,2017 katika Makao Makuu ya Ofisi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) iliyopo mtaa wa Ufipa wilaya ya Kinondoni, Mdee anadaiwa kutamka maneno dhidi ya  Rais John Magufuli kuwa  “anaongea hovyohovyo , anatakiwa  afungwe breki”  na kwamba kitendo ambacho kingeweza  kusababisha uvunjifu wa amani.  

Mdee alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Julai 10, 2017 na yupo nje kwa dhamana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...