Na Ahmed Mahmoud Arusha 

Wabunge wa Tanzania kwenye bunge la Afrika mashariki wametoka nje ya bunge akigomea kuletwa kwa muswada wa mabadiliko ya sheria za bandari ambao hauna maslahi na taifa letu. 

Akiongea nje ya ukumbi wa bunge hilo Mariamu Ussi Yahaya alisema kuwa muswada huo unaotakiwa kuletwa utaounguza mapato ya bandari zetu hivyo hauna maslahi kwa taifa letu. 

Alieleza kuwa nchi zenye bandari kwenye jumuiya hiyo ni Tanzania na Kenya hivyo kuletwa kwake ndani ya bunge kwa wakati huu sio sahihi una lengo la kuhujumu mapato yetu kama taifa 

Aliwambia kuwa Hatukatai muswada huu kama nchi kwa kuwa bado kuna takiwa kufanyika kwa mapitio na upembuzi kabla haujaletwa bungeni kujadiliwa lakini tunaona unataka kuletwa bunge kabla haujafanyiwa upembuzi kwani sheria hii ilikuwepo awali. 

“Tumeamua kutoka nje baada ya kuona Kuna muswada wa sheria ambao hauna nia nzuri kwani sheria zipo na zinaweza kubadilishwa lakini sio kwa wakati huu” Muswada mbalimbali imajadiliwa tokea kuanza kwa bunge hilo wiki iliyopita ikiwemo kusomwa kwa taarifa ya ukaguzi wa fedha za jumuiya hiyo iliyowasilishwa bungeni humo na mbunge na Mwenyekiti wa kamati ya Fedha ya bunge hilo Dkt.Ngwaru Maghembe na kueleza kuwa kumekuwa na mafanikio makubwa tofauti na mwaka uliopita kwenye matumizi ya jumuiya. 

Hali hiyo imeonyesha kuongezeka kwa ubanaji wa matumizi ya shughuli za jumuiya hiyo kama agizo la Mwenyekiti wa wakati huo Dkt.John Magufuli alivyoahidi hali hiyo imepelekea mwaka huu jumuiya hiyo kupata hati safi tofauti na mwaka uliopita. 

Bunge hilo linalotarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwezi huu tarehe 29 limekuwa na mijadala mikali inayoendelea hali iliyopelekea Jana wabunge watanzania kutoka nje ya ukumbi wakigomea kuletwa kwa muswada wa mabadiliko ya sheria za bandari ambazo wao wanaona hazina maslahi mazuri na kwa taifa na itapunguza mapato ya bandari zetu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...