Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Wajasiriamali wanaozalishaji wa bidhaa mbalimbali zinzotumia kemikali wametakiwa kutumia kemikali hizo kwa usalama ili ziweze kuleta madhara kwa  watumiaji na wakati mwingine madhara hayo yanaweza kutokea hata kwa wazalishaji.

Akizungumza  katika Mafunzo ya wajasiriamali wa Wadogo na Kati wa Kanda ya Mashariki  yaliyofanyika  jijini Dar es Salaam Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko amesema kuwa uchumi wa viwanda nchini pamoja na wazalishaji  wa bidhaa wanaotumia kemikali wanahitaji kuwa na matumizi salama ya kemikali hizo.

Dkt.Mafumiko amesema kuwa kemikali zisipotumika kwa usahihi zinaweza kuleta madhara ya kimazingira ambapo athari zake ni kubwa  ambapo maendeleo yanayohitajika yasiweze kufikiwa.

Amesema kuwa wananchi wanauelewa wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) kwa kutokana na kujisajili vibali vya uingizaji wa bidhaa za kemikali nchini hivyo watumiaji nao lazima wawe na elimu ya utumiaji wa Kemikali hizo katika uzalishaji wa bidhaa.

“GCLA inataka wajasiriamali waendelee ni pamoja na kutumia kemikali kwa usahihi wake ili zisiweze kuleta madhara kwa wananchi  kutokana na kutumia bidhaa ambazo kemikali zake hazijatumika kwa taratibu zinazotakiwa”amesema  Dkt.Mafumiko

Dkt.Mafumiko amesema kuwa mafunzo mengine yatakwenda kwa wauzaji wa kemikali ambao wanatakiwa kuuza bidhaa za kemikali zilizo bora na si vinginevyo .

Mkurugenzi wa Sabuni za Usafi Majumbani na Viwandani Jovita Masanyika amesema kuwa Mafunzo hayo ni muhimu kwao kwani ndio watumiaji wa kemikali katika uzalishaji wa bidhaa mbalimbali.

Amesema kuwa elimu walioipata wataitumia katika utengenezaji wa bidhaa bora kwa kuzingatia matumizi salama ya kemikali na kuongeza kuwa wauzaji nao wanatakiwa kupewa elimu hiyo.

Mkufunzi wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) George Buchafwe amesema kuwa SIDO itaendelea kushirikiana na GCLA katika kuhakikisha wajasiriamali wanafikia viwango vinavyohitajika katika matumizi ya kemikali.
 Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt.Fidelice Mafumiko akizungumza katika mafunzo ya  Wajasiriamali wa Kanda wa Mashariki kuhusiana na matumizi sahihi ya Kemikali yaliyfanyika katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Kemikali  wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali(GCLA) Daniel Ndiyo akitoa maelezo wakati akiwakilisha mada kwa wajasiriamali wa kanda ya mashariki iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkufunzi wa Shirika la Kuhudumia  Viwanda Vidogo (SIDO) George Buchafwe akizungumza namna wanavyowaratibu wajasiriamali  katika uanzishaji wa wa viwanda namana ya kufuata taratibu za serikali.
 Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt.Fidelice Mafumiko akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana Mamlaka hiyo inavyodhibiti kemikali nchini zisiweze kutumika vinginevyo wakati wa mafunzo kwa wajasiriamali wa Kanda ya Mashariki yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Sabuni ya Usafi Jovita Masanyika akizungumza namna wanavyotumia kemikali katika uaandaji wa bidhaa za sabuni wakati wa mafunzo kwa wajasiriamali wa Kanda ya Mashariki yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mjasiriamali wa Sabuni Maria Lwila akitoa maelezo kuhusiana na upatikanaji wa kemikali  wakati wa mafunzo kwa wajasiriamali wa Kanda ya Mashariki yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt.Fidelice Mafumiko  akiwa katika picha ya pamoja na wajasiriamali wa Kanda ya Mashariki  mara baada ya kufungua mafunzo ya kwa wajasiriamali hao

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...