Na Karama Kenyunko, Michuzi Globu 

WAKILI Nyaronyo Kicheele anayemtetea mshtakiwa Samwel Philemon anayekabiliwa na kosa la kulawiti ameomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufungua akaunti za mteja wake zinashoshikiliwa na polisi kwani mashtaka yanayomkabili siyo ya uhujumu uchumi na wala hayahusiani na fedha.


Kicheele amewasilisha maombi hayo leo Februari 17,mwaka 2020 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Rashid Chaungu wakati mshtakiwa Philemon ambaye ni mfanyabiashara na mwenzake ambaye ni video Queen Aisha Juma maarufu kama Candy walipofikishwa mahakamani hapo kusomewa shtaka la kusambaza picha za ngono na kulawiti.


Kabla ya maombi hayo, Wakili wa Serikali Kija Ruzungana aliwasome washtakiwa makosa yao ambapo amedai Desemba 12, 2019 jijini dar es Salaam mshtakiwa Aisha alisambaza picha za ngono kupitia mtandao. Aidha katika siku na mahali pasipojulikana mshtakiwa Philemon alimlawiti mshtakiwa mwenzio huyo Aisha binti wa miaka 19 huku akijua kufanya hivyo ni kosa.


Mara baada ya kusomewa shtaka lao Wakili Kicheele alidai, "mshtakiwa Philemon anashtakiwa kwa kosa la kulawiti, ni kosa ambalo halihusiani na uhujumu uchumi wala fedha, si wizi wala ujambazi lakini akaunti zake za benki zimefungiwa.... mshtakiwa ni baba wa watoto na pia ana mke na wazazi wanamtegemea" amedai Kicheele ma kuongeza "tunaomba akaunti zake za benki zifunguliwe ili familia yake iweze kula maana sasa hivi wamekuwa omba omba kama chokoraa. 


Akijibu hoja hiyo Wakili wa Serikali Kija amedai kwa sasa hawezi kulizungumzia hilo  suala la akaunti kwa kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na hatujui kama mshtakiwa ana kesi nyingine ama hizo akaunti ni sehemu ya ushahidi ndio maana wameshilia ama la hivyo ameomba wapatiwe muda waweze kufuatilia hilo.


Hata hivyo Hakimu Chaungu amesema anashindwa kuto amri ya kuwataka waeleze kwa nn akaunti za mshtakiwa zimefungiwa ila amewataka upande wa Jamuhuri tarehe inayokuja waje waeleze kwa nini akaunti hizo zimefungiwa.


Washtakiwa wote wamekana kutenda makosa yao na wamerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana yaliyowataka kuwa na wadhamini wawili kwenye barua na kitambulisho chochote ambao wameweka bondi ya sh. Milioni 10. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 26 mwaka huu.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...