Janeth Maro akielezea namna ambavyo wanaandaa mbolea ambayo si ya kemikali kwa ajili ya kuweka kwenye mazao mbalimbali
Moja ya bwawa kubwa la maji lenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni 12 kwa ajili ya kumwagilia mazao yaliwepo kwenye Kituo cha Utafito cha SAT
Mkurugenzi Mtendaji wa SAT Janeth Maro akionesha miti ambayo inatumika kurejesha rotuba kwenye ardhi ili mazao yanayopandwa yaweze kustawi


Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kilimo Endelevu Tanzania(SAT) Janeth Maro akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu kilimo cha Rozela.
Meneja wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha SAT Frank Marwa akiwa ameshika mmea wa Rozela wakati anaelezea namna ambavyo kituo hicho kinavyolima zao hilo ambalo soko lao kubwa liko nchini Uswis. 
 
 
Na Said Mwishehe, Michuzi Globu ya jamii

WAKULIMA nchini Tanzania wameshauri kuchangamkia fursa ya zao la Rozela katika masoko kwa kulima kwa wingi zao hilo kwa njia ya Kilimo hai kwani linalipa na halimtupi mkulima.

Ushauri huo umetolewa na Mkurugezi wa Shirika la Kilimo endelevu Tanzania (SAT) Janeth Maro, wakati akizungumza na waandishi wa habari waliokuwa kwenye ziara ya mafunzo ya Kilimo hai kwenye Taasisi ya utafiti wa kilimo hai inayomilikiwa na Shirika hilo wilayani Mvomero, Morogoro.

Amesema zao la rozela ni moja ya zao lenye soko kubwa ndani na nje ya nchi na wakulima wengi hawajui fursa zilizopo kwenye zao hilo. "Moja ya jukumu letu ni kuonesha fursa zilizopo katika kilimo hai, hivyo nitoe rai kwa wakulima kujikita pia kwenye kilimo cha rozela kwani soko lake ni la uhakika na hasa nje ya nchi."

Amefafanua Rozela ya Tanzania ina soko kubwa sana nje ya nchi hasa kwenye nchi ya Uswisi ambapo TAS imekuwa ikipeleka zao hilo wanalolima kwenye kituo chao kwa njia ya asili."Tumepata soko zuri Uswisi na hata hapa ndani ya Tanzania, kwa sasa tupo hatua ya mwisho ya kupeleka rozera tuliyoifungwa kwenye pakiti 5000 na inauzwa kwa bei nzuri," anasema .

Amesema kuwa wao wanauza Rozela kwa pakiti ndogo ya gramu 50 kwa dola tano ambayo ni sawa na Sh.2700, hivyo wakulima wajaribu kuangalia fursa zilizopo kwenye zao hilo.

Wakati huo huo amesema mazao mengine yenye soko nchini Uswisi ni pamoja na mazao ya viungo, mdarasini na pilipili manga ambapo pia wapo kwenye hatua ya mwisho kupeleka nchini humo tani 10 mpaka 15.

Amesema zao hilo halina ugumu kwenye kulima kwa kuwa linapaliliwa tu na linaota na kustawi kwenye mvua chache hasa ikinyesha wakati wa kukaribia mavuno."Kwa Tanzania zao hilo linastawi zaidi kwenye maneo kama Mvomero ambapo kuna mvua ndogo kwa mwaka na maeneo mengine yenye hali kama ya wilaya hiyo.

Kwa upande wake Meneja wa kituo cha utafiti wa Kilimo hai cha SAT Frank Marwa, amesema kuwa Rozera ni zao muhimu kwa maisha ya binadamu ambapo faida yake kubwa ni kwamba ina chembechembe za kuondoa sumu mwilini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 31, 2021

    Ninampango wa kulima lozela msimu wa 21/22 mnanihakishiaje soko?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...