Na Jusline Marco-Arusha

Zaidi ya wanafunzi 200 walio katika shule ya sekondari Kitefu Wilayani Arumeru wamepatiwa elimu ya afya ya uzazi itakayo wasaidie kuepuka mimba za utotoni na kuwezesha kufikia malengo yao kielimu.

Elimu hiyo ambayo imetolewa na shirika la Center for women and Girls Empowerment kutoka Mkoani Arusha ni kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya wanafunzi wanaopata mimba za utotoni kutokana kutopata elimu ambayo itamuwezesha kujikinga na mimba za utotoni.

Akizungumza katika zoezi la ugawaji wa taulo za kike katika shule hiyo Dkt.Waziri Njau Mratibu wa mradi wa tupange pamoja Kanda ya Arusha kutoka katika Shirika la Jhpiego ambao unatoa elimu kwa vijana kuhusiana na afya ya uzazi pamoja na huduma rafiki kwa vijana amesema kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali wameweza kuonyesha upendo kwa mtoto wa kike kwa kutoa elimu ya afya ya uzazi itakayomsaidia kujikinga na mimba za utotoni.

Aidha amesema kuwa kama mtoto wa kike anapaswa kujua namna gani ya kutunza mwili wake wakati wa hedhi ili kuweza kuepuka magonjwa katika via vya uzazi yatokanayo na uchafu ikiwemo ugonjwa wa fangasi ikiwa ni sambamba na kuepuka mimba za utotoni kwa kuzuia miili yao kutoingia kwenye tamaa.

Vilevile ameongeza kuwa vifo vya akina mama na watoto vinavyotokea wengi wao ni wanawake wenye umri chini ya miaka 24 na idadi hiyo imetokea kutokana na mimba za utotoni ambapo ametoa wito kwa wazazi na walezi kuwa karibu na kuwafundisha watoto wao njia sahihi za kuepuka vishawishi na hatimaye kufikia ndoto zao.

Pamoja na hayo amesema kuwa kutokana na idadi ya watumiaji wa dawa za dharura kubwa,mashirika hayo yameamua kutoa elimu ya huduma rafiki kwa vijana mashuleni ili iweze kuwasaidia endapo elimu ya makuzi na stadi za maida itakuwa imewafikia vijana ambapo mpaka sasa wauzaji wa maduka yapatayo 400 ya dawa za binadamu wamepatiwa mafunzo iliwaweze kutoa huduma stahiki kwa watu sahihi.


Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Center for women and Girls Empowerment Hilda Kinambo amesema kuwa lengo la ugawaji wa taulo za kike pamoja na utoaji wa elimu ya afya ya uzazi imetokana na uwepo wa uhitaji mkubwa wa taulo za kike kwa wanafunzi walio katika maeneo ya vijijini.

"Kwa mujibu wa taarifa ambazo nilizipokea kutoka kwa mwalimu mkuu ni watoto ambao wanatoka kwenye familia ambazo wanamazingira magumu kwahiyo tukaona jinsi gani kama sisi Center For Women tunaweza kumuinua mtoto wa kike ili aweze kujisikia uhuru na kuweza kusoma katika mazingira ambayo ni salama hivyo tukaona tuanze kwa kuweza kumletea mtoto wa kike taulo za kike na kutoa elimu kuhusiana na masuala ya afya ya uzazi na kuwajengea uwezo wa kujiamini na kusimama kinyume na kila kitu ambacho ni uovu katika jamii inayomzunguka." Alisema Bi.Hilda

Ameongeza kuwa kutokana na ongezeko la mimba za utotoni kuwa kubwa ni lazima jamii ifikie hatua ya kuzuia watoto wa kike kwa kuwapatia elimu hiyo kulingana na kauli mbiu ya kampeni hiyo inayosema MPENDE MFANYE AJIAMINI KWA KUMUELIMISHA.


Naye Mkurugenzi wa kampuni ya Tulip Water Filter Tanzania ikiambatana na Afripads Bi.Rephrin Allan Kombe amesema kuwa kampeni hiyo taulo hizo za kike zitawasaidia wanafunzi hao kujisitiri kwa muda wa mwaka mmoja kwa kuzifua baada ya kuzitumia ambazi zitafanya wawe huru zaidi wakati wa hedhi.

Pamoja na hayo mmoja wa waandaaji katika kampeni hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa taasisi ya Voice of Youth Bwn.Vicent Uwega amesema kuwa wameamua kusambaza upendo kwa kutoa elimu ya jinsia kwa wanafunzi wasichana walio katika shule zilizo nje ya mji katika kuhakikisha wanafikiwa hiyo kama sehemu ya kuwasaidia.

Amebainisha kuwa elimu ya malezi na makuzi zitawasaidia wanafunzi hao kujikinga na kuepuka mimba za utotoni ambazo zinaweza zikahatarisha usalama wa maisha yao na kukatiza masomo yao.
   Picha ya pamoja wadau na wanafunzi wa shule ya aekondari Kitefu waliopewa taulo za kike wakifurahia zawadi hizo.
Wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha nne katika Shule ya Sekondari Kitefu Wilayani Arumeru,Mkoani Arusha wakifuatilia kwa makini elimu ya afya ya uzazi  iliyotolewa na Taasisi ya Center for Woman and Girls kupitia kampeni ya MPENDE,MFANYE AJIAMINI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...