Charles James, Michuzi TV

SERIKALI imesema mwisho wa wanafunzi wanaotembea umbali mrefu kwenda shule katika kata ya Nala jijini Dodoma ni mwaka huu kwani kuanzia mwakani hakutakua na changamoto ya madarasani katika shule ya msingi kwenye kata hiyo.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Mhe Selemani Jafo wakati akizindua shule shikizi ya msingi ya Chiwondo iliyopo katika Jiji la Dodoma.

Shule hiyo imejengwa kwa msaada wa Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Mhe Anthony Mavunde kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji hilo ambapo tayari vyumba vinne vya madarasa vimeshakamilika huku vingine vitatu vikiwa kwenye ujenzi.

Akizungumza na viongozi, wananchi na wanafunzi waliojitokeza kwenye uzinduzi huo, Mhe Jafo amemuagiza Mkurugenzi wa Elimu-Tamisemi, Bw Julius Nestory kuhakikisha Shule hiyo inaongezewa madarasa mawili kabla ya kuanza kwa Bunge lijalo la bajeti.

" Kazi kubwa ambayo imeoneshwa na Mbunge wenu inapaswa kuungwa mkono na kila mmoja wetu, hivyo nakuagiza Mkurugenzi wa Elimu uhakikishe ujenzi wa madarasa mawili unaanza mara moja kabla ya bunge la bajeti kuanza.

Hatuwezi kumuachia  Mbunge peke yake kazi ya kuleta maendeleo, lakini pia nakuagiza Mkurugenzi uhakikishe katika ajira zijazo za serikali Shule hii inapata walimu na kuondoka na na changamoto ya walimu iliyopo," Amesema Mhe Jafo.

Amesifu jitihada kubwa zilizooneshwa na Mbunge Mavunde za kuinua elimu kwenye jimbo lake na kuwataka wananchi, wazazi kukubaliana nae kuiita shule hiyo jina la Mavunde.

" Mimi hizi shule zipo kwenye mamlaka yangu nimesikia mnasema inaitwa Chiwondo mimi naagiza isajiliwe kwa jina la Mavunde, hii ndiyo heshima pekee ambayo tunaweza kumpa Mbunge wetu," Amesema Jafo.

Kwa upande wake Mhe Mavunde amemshukuru Waziri Jafo na viongozi wengine waliofika kwenye uzinduzi huo kwani kukamilika kwa shule hiyo kumepunguza changamoto ya umbali mrefu iliyokua ikiwakabili wanafunzi hao.

" Mhe Waziri kabla ya shule hii iliwalazimu wanafunzi hawa watoto kutembea Km 20 kila siku kwenda na kurudi shuleni, jambo ambalo kwa hakika lilisababisha wengi wao kuacha shule na wengine kufanya vibaya kutokana na uchovu wanaoupata," Amesema Mavunde.

Akizungumza na Michuzi Blog mara baada ya kuzinduliwa kwa shule hiyo mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo, Anneth Jacob amemshukuru Mhe Mavunde kwa kuwaletea shule hiyo kwani anaamini itakua safari ya wengi kutimiza ndoto zao za kimasomo na kimaisha.

Kufunguliwa kwa shule hiyo shikizi kumeongeza idadi ya wanafunzi waliojiunga na elimu ya awali kutoka 15 waliokua wakisoma Chihoni hadi 63 sasa wanaosoma Chiwondo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Selemani Jafo akizindua shule shikizi ya Chiwondo. Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi, Mkurugenzi wa Jiji, Godwin Kunambi na Mbunge wa Jimbo hilo, Anthony Mavunde.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo (katikati) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge (kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde kwenye moja ya madarasa ya shule shikizi iliyozinduliwa leo.
 Wananchi mbalimbali waliojitokeza kwenye uzinduzi wa shule shikizi ya msingi iliyopo katika kata ya Nala ambayo imezinduliwa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Selemani Jafo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Selemani Jafo, Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde na wadau wa elimu kutoka taasisi ya GFF wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya wadau hao kukabidhi madawati 60 kwa ajili ya kusaidia shule hiyo shikizi.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Selemani Jafo akizindua shule shikizi ya Chiwondo. Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi, Mkurugenzi wa Jiji, Godwin Kunambi na Mbunge wa Jimbo hilo, Anthony Mavunde.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...