Na Woinde Shizza, Arusha

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Zelote Stephen amewatumia salaam za onyo kali baadhi ya viongozi na wanachama wa Chama hicho mkoani Arusha ambao bado wameendelea kukaidi agizo lake alilolitoa mara tu baada ya kuchaguliwa kwenye nafasi hiyo la kuvunja makundi ndani ya saa 48.

Zelothe ametuma salam hiz0 wakati akifungua mkutano wa halmashauri kuu ya Chama cha mapinduzi wilaya ya Ngorongoro na kusema kuwa licha ya kuwa maelekezo yake yametekelezwa kwa asilimia kubwa bado wapo wanachama na viongozi wachache mkoani humo wanaoweweseka wakijaribu kuendeleza makundi na kuwachafua baadhi ya viongozi jambo ambalo amewatahadharisha katika uongozi wake hawana nafasi.

"napenda kuwaambia baadhi ya viongozi na wanachama Wa chama cha mapinduzi ambapo wanamakundi wanakazi ya kuwachafua viongozi waache Mara moja nilitoa mda lakini naona kunabaadho hawasikii ,niwaambie waache au waondoke maana kwenye uongozi wangu hakuna nafasi " alibainisha Zelote STEPHEN …Mwenyekiti CCM mkoa wa Arusha

Kwa upande wake Mwenyekiti Wa chama cha mapinduzi wilaya ya Ngorongoro Durango Senge alisema kuwa lazima walinde juhudi na Kazi zinazofanywa na Rais magufuli na hawatakubali kuona MTU yeyote yole anachafua Kazi nzuri anazozifanya Rais ,huku akisema kuwa hakuna kiongozi yeyote ambaye alishawahi kushika madaraka akapelek huduma mbalimbali kama shule na hospital kwa kipindi kimoja.

Naye naibu Waziri Wa Elimu William Ole Nasha alisema katika miaka mitano ya serikali ya Rais Magufuli kwa upande Wa ngorongoro wamepata neema kubwa ya kuingia kwenye miradi mikubwa ya kimaendeleo ,alibainisha kunamiradi mikubwa ambayo inatekelezwa na fedha nyingi za kuleta maendeleo zimepelekwa katika halmashauri ya ngorongoro ,hivyo aliipongeza serikali na kisema kuwa maendeleo kufanikiwa ni jitihada za watu wengi.

Aliwataka waendeshe chama kufuata taratibu na sharia wasiwe wanachama Wa kuongoza chama kwa vipeperushi, wasiwe wasifanye Siasa za maji taka Bali wafanye Siasa za kueleweka pamoja ya kwamba ngorongoro inachangamoto nyingi ya kijegrafia waendelee kuwa wamoja na wajitume zaidi.

Katika kikao hicho kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro,mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro, baraza la wafugaji Ngorongoro na mbunge wa jimbo hilo Willium Ole Nasha waliwasilisha taarifa za utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM kwa 2015 -2020 katika miradi mbalimbali ya maendeleo.


Katika kikao hicho mwenyekiti wa CCM mkoa pia aliipongeza serikali ikiongozwa na mkuu wa mkoa huo Mrisho Gambo kwa ushirikiano mzuri uliopo baina ya Chama na serikali katika utekelezaji wa Ilani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...