Na Amiri Kilagalila-Njombe

Watu saba wamepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Njombe na kusomewa mashtaka 12 moja kati ya hayo ni la uhujumu uchumi na makosa 11 ya wizi wa mali za muungano wa vyama vya wakulima wa chai lupembe mvyulu.

Mwanasheria wa serikali Matiku Nyangero amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Jachindus Mkolwe[73],Bossy Mbanga[60],Andrew Ulungi [57],Henrick Lupembe[67],Abakuki Mhomisoli[49],Martin Mtali[65] na Acrey Mfugale[38] ambao wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya januari 2008 na januari 2020.

Aidha watuhumiwa hao wamefunguliwa kesi ya uhujumu uchumi kwa kukusababishia hasara mamlaka ambacho ni chama cha wakulima wa chai lupembe mvyulu kwa kesi namba 4 ya mwaka 2020  kinyume na paragrafu ya kumi ndogo ya kwanza jedwali la kwanza kifungu cha 57 kidogo cha kwanza na kifungu cha 60 kidogo cha kwanza.

Mwanasheria huyo amesema watuhumiwa hao kwa pamoja walijihusisha na wizi wa mali za mvyulu zikiwemo mashine motors za kiwanda cha chai cha igombola,generator tofauti tofauti pamoja na injini za mashine ambazo zote kwa pamoja zina thamani ya shilingi milioni 819,050,000.

Amesema makosa hayo ya wizi wa mali mbalimbali yapo chini ya kifungu cha 258[1] na kifungu cha 265 cha kanuni ya adhabu sura  no 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Hakimu mkazi wa mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa njombe hassan makube amesema mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi za uhujumu uchumi na hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kuzungumza chochote na kesi hiyo imeahirishwa hadi februari 17 mwaka huu itakapotajwa tena na washtakiwa wamerejeshwa rumande.

Hata hivyo watuhumiwa hao waliwekwa korokoroni kwa maelekezo ya naibu waziri wa kilimo chakula na ushirika Hussein Bashe baada ya kuzulu katika kiwanda cha chai Igombola Lupembe hapo januari 11 mwaka huu ambako alikutana na pande zote mbili za wakulima wa chai chini ya Mvyulu na mwekezaji wa kiwanda hicho Yusuph Muller huku akiivunja bodi ya mvyulu pamoja na kuelekeza mali zote zitafutwe popote zilipo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...