Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala(kushoto) akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(kulia) na Watumishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyapori(TAWA), Wakala wa Huduma za Mistu Tanzania (TFS) Kanda ya Magharibi na Hifadhi za Taifa(TANAPA) jana mara baada ya ziara yake ya kikazi Mkoani humo.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala, Mkuu wa Mkoa wa Tabora aggrey Mwanri , Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu na Watendaji wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyapori(TAWA), Wakala wa Huduma za Mistu Tanzania (TFS) Kanda ya Magharibi na Hifadhi za Taifa(TANAPA) wakiwa katika picha ya pamoja jana kabla hajaanza  ziara yake ya siku moja ya kikazi Mkoani Tabora.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala akisamiliana jana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Adam Malunkwi wakati alipowasili katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Urambo kwa ajili ya kuanza ziara ya kutembelea eneo lenye mgogogo katika Maliasili na wakati wa Kata ya Nsenda.
Mkuu wa Wilaya ya Urambo Angelina Kwingwa akitoa taarifa ya Wilaya kwa Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala wakati alipowasili kwa ajili ya kuanza ziara ya kutembelea eneo lenye mgogogo katika Maliasili na wakati wa Kata ya Nsenda. 
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala akizungumza na viongozi mbalimbali wa Wilaya na wale wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo wakati alipowasili kwa ajili ya kuanza ziara ya kutembelea eneo lenye mgogogo katika Maliasili na wakati wa Kata ya Nsenda.
Na Mpiga picha wetu
………………………………………………………………………………………………….
NA TIGANYA VINCENT
WATUMISHI wa Mamlaka na Wakala zilizopo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii wametakiwa kuhamia katika maeneo ya hifadhi ili kulinda na kuzuia uharibifu wa maliasili kwa ajili ya maendeleo ya Nchi.
Kauli hiyo imetolewa  na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala wakati akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Tabora , Watumishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyapori(TAWA), Wakala wa Huduma za Mistu Tanzania (TFS) Kanda ya Magharibi na Hifadhi za Taifa(TANAPA) kwenye ziara yake ya kikazi.
Alisema Taasisi zote zinahusika na usimamizi na ulinzi wa  maliasili zinatakiwa kujenga Ofisi ndani ya Hifadhi na watumishi kuhamia huko ili iwe rahisi kukabiliana na uharibifu wowote unaotaka kufanyika.
Dkt. Kigwangala aliongeza katika Ofisi zilizopo nje ya hifadhi wabaki watumishi wachache ikiwemo Watendaji wakuu na waliobaki waende porini kwa kuwa tayari walishapata mafunzo ya jinsi ya kupambana na waharibifu wa maliasili.
“Hatuwezi kulinda maliasili tukiwa maofisini …ni lazima tujenge post kwenye hifadhi zetu na watumishi wahamie huko wakalinde maliasili zetu , ofisi wabaki wachache ikiwemo viongozi wa Kanda… wao watakwenda kukagua utendaji kazi wa watumishi wanaowasimamia” alisisitiza
Alisema ni jukumu lao kuhakikisha maliasili zilipo ikiwemo wanyamapori , ndege na mimea inalindwa kwa ajili ya faida ya kizazi cha sasa na kijacho na kuhakikisha wanazuia uharibifu wowote ndani ya Hifadhi nchini.
Waziri huyo alisema kuwa Kanda ya Magharibi ndio pekee imebaki na mistu mingi ya asili ni vema watendaji wanaohusika kulinda na kuhifadhi wakahakikisha haiendelei kuharibiwa.
Katika hatua nyingine Dkt. Kigwangala ametoa siku 14 kwa Taasisi zilizopo chini Wizara ya Maliasili na Utalii katika kanda ya Magharibi kukaa pamoja na kuanisha mipaka halisi ya Hifadhi mpya za Taifa, mapori ya akiba na Hifadhi ya Mistu  na maeneo ya wananchi ili kuondoa mwingiliano na migogoro.
Alisema kumekuwepo na mlingiliano ambao umetokana na baadhi ya maeneo ya hifadhi moja kusomeka katika eneo jingine la hifadhi na kuleta utata.
Aidha Dkt. Kigwangala alizitaka Taasisi hizo kuhakikisha wanaweka upya mipaka katika Msitu wa Hifadhi wa Ulyankulu ambapo kuna sehemu ambayo wananchi wameshavamia na kufanya makazi na kujenga huduma mbalimbali.
Alisema mipaka hiyo itasaidia wananchi kuendelea kuingia katika msitu huo na kuendesha shughuli mbalimbali ambazo zinatishia uendelevu wa msitu huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...