WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amelitaka Jeshi la Polisi kuangalia aina ya makosa ya watuhumiwa ambayo yana dhaminika ili kupunguza mlundikano wa mahabusu Magerezani.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukagua miradi ya maendeleo ya Jeshi la Magereza na baadaye kuzungumza na Maafisa na Askari wa Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dodoma, leo, Simbachawene alisema Jeshi hilo linakabiliwa na changamoto ya idadi kubwa ya mahabusu ukilinganisha na wafungwa waliopo magerezani.
“Mlundikano wa mahabusu magerezani ni changamoto kubwa, lakini inapaswa kuangaliwa kwa upana zaidi, hasa kwa Jeshi la Polisi kuangalia makosa yanayodhaminika ili wasizalishe mahabusu kwasababu zisizo za msingi,” alisema Simbachawene.
Aliongeza kuwa, kwa kufanya hivyo kutasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza msongamano magerezani sambamba na kuipunguzia Serikali gharama ya kuwahudumia wafungwa na mahabusu.
“Tunajaza magereza yetu kwa kuzalisha mahabusu kwa makosa ambayo mengine hayastahili kuwaleta magerezani kama vile ugomvi wa kifamilia na makosa mengine madogo madogo ambayo yanadhaminika,” alisisitiza Simbachawene.
Aidha, akitoa taarifa ya Jeshi hilo, Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP), Suleiman Mzee alisema kwasasa kuna wafungwa 14,502 na mahabusu 17,396 katika magereza yote nchini.
“Tutajitahidi kuendelea kushirikiana kwa pamoja katika jukwaa letu la haki jinai ili kuangalia namna bora ya kutatua tatizo au changamoto ya msongamano wa mahabusu magerezani,” alisema Kamishna Jenerali Mzee.
Kamshina Jenerali Mzee alimshukuru Waziri Simbachawene kwa kufanya ziara Makao Makuu ya Magereza na kuahidi kuyafanyia kazi maagizo mbalimbali aliyoyatoa kwa Jeshi hilo ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akitoa maelekezo kwa Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Suleman Mzee(kulia) leo alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, jijini Dodoma ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu ateuliwe katika Wizara hiyo.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akizungumza na Maafisa na askari wa Jeshi la Magereza(hawapo pichani)leo alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, jijini Dodoma ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu ateuliwe katika Wizara hiyo. Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Suleman Mzee( Kulia )ni Kamishna wa Utawala na Rasilimali watu, Uwesu Ngarama.
 Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Suleiman Mzee akitoa taarifa fupi mbele ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene(meza kuu katikati) kabla ya kuongea na Maafisa na askari wa Jeshin hilo. Kulia ni Kamishna wa Utawala na Rasilimali watu, Uwesu Ngarama.
 Baadhi ya Maafisa na askari wa Jeshi la Magereza Mkoani Dodoma wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, George Simbachawene (hayupo pichani).
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene(kulia) akitoa maelekezo kwa Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Suleman Mzee(wa pili toka kushoto) leo alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, jijini Dodoma ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu ateuliwe katika Wizara hiyo.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene(Kaunda suti) akiingia Gereza Kuu la Isanga, jijini Dodoma, leo, tayari kwa kuzungumza na Wafungwa na Mahabusu waliopo katika Gereza hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...