Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi (wa pili kushoto) akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu (kushoto) aliyefika ofisni kwake, Zanzibar kwa ajili ya kujitambulisha baada ya kuteuliwa hivi karibuni kushika nafasi hiyo. Wengine pichani ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohamed Aboud na Mkurugenzi wa Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohamed Aboud na Mkurugenzi wa Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk wakiwa katika kikao na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi alipokutana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu ofisini kwake, Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akisaini kitabu cha wageni alipowasili Ofisi ya Makamu wa Rais iliyoko Zanzibar na kujitambulisha kwa watumishi wa Ofisi hiyo ikiwa ni baada ya kuteuliwa hivi karibuni.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akizungumza na watumishi wa Ofisi hiyo upande wa Zanzibar alipofanya ziara visiwani humo kwa ajili ya kujitambulisha baada ya kuteuliwa hivi karibuni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...