Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa amewatahadharisha nchi ya Zambia kuacha mara moja kuzuia magari yanayotoka Tanzania kupeleka mahindi nchi ya Kidemokrasia Congo.

Hatua hiyo imekuja baada ya malalamiko ya wafanyabiashara na wasafirishaji wa mahindi kuelekea nchini Congo kuzuiliwa katika mpaka wa Tunduma.

Bashungwa amesema kuwa anafahamu changamoto wanayokutana nayo pale mtaani ila kwa sasa wanataka kulimaliza jambo hilo kidiplomasia na tayari wameshamuagiza Balozi wa Tanzania nchini Zambia kushughulikia hilo.

",Ni kweli tunafahamu changamoto mnayoipata mnapofika mpakani, Wanawazuia kuingia nchini mwao ila kwetu sisi wanapita, tumeshatoa maagizo kwa Balozi wa Tanzania nchini mwao aweze kuzungumza nao na sisi tunataka kulimaliza suala hili kidiplomasia kabla hatujachukua maamuzi mengine,"amesema

Bashungwa amesema, "Zambia magari yao yanapita bila kuzuiliwa au kusumbuliwa wakiwa wanapeleka bidhaa zao nchini Rwanda ila kama watataka na sisi tuyazuie tutafanya hivyo ila kwa sasa tunataka tulimalize kidiplomasia"

Aidha, amewaomba wafanyabiashara na wasafirishaji kuwa na uvumilivu kwenye kipindi hiki cha mariadhiano kabla ya serikali kufanya maamuzi yoyote au kutoa tamko.

Wasafirishaji hao wametoa malalamiko yao kwa Waziri husika kuweza kushughulikia changamoto ya kuzuiliwa kwao kupita mpakani mwa Tanzania na Zambia wakati wanasafirisha mahindi kwenye nchini Congo na hata kufikia kukaa kwa muda wa miezi miwili na wao wakipita bila usumbufu wowote.
Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa akielezea mkakati wa serikali katika kuwasaidia wafanyabiashara na wasafirshaji wa Mahindi kwenye nchi ya Kidemokrasia Congo na kuzuiliwa mpakani mwa Tanzania na Zambia. Kulia ni Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe na Waziri wa Ufugaji na Uvuvi Luhaga Mpina wakati wa Mkutano wa wadau wa sekta za Kilimo, Ufugaji na Uvuvi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...