Benki ya NMB katika kudhibiti na kupambana dhidi ya virusi vya Corona imekabidhi shilingi milioni 100 kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kama sehemu ya mchango wake kwa serikali katika mapambano hayo.
Waziri mkuu amekabidhiwa fedha hizo na Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya NMB-Ruth Zaipuna mwishoni mwa wiki katika ofisi ya Waziri Mkuu, Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (wa tatu kushoto) akipokea hundi ya Sh. Milioni 100 kwa ajili ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (wa nne kutoka kushoto) Kushoto ni Afisa Mkuu wa Wateja Wakubwa wa Serikali wa NMB Alfred Shao na kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.
Waziri Mkuu- Kassim Majaliwa akizungumza na uongozi wa Benki ya NMB

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...