Mkurugenzi wa Teknohama na
Uendeshaji wa benki ya TPB Jema Msuya (kushoto) akikabidhi mifuko 200 ya saruji
yenye thamani ya shilingi milioni 3.7 kwa Mbunge wa CCM Viti Maalum Mkoa wa Rukwa Bupe Mwakang’ata
kwa ajili ya kusaidia ukamilishaji wa ujenzi wa madarasa ya shule mbalimbali
Mkoani hapo. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa Reiner Rukalah na
Mwenyekiti wa UWT Mkoa Maria Kalula. 

Mbunge wa Viti Maalum wa
Rukwa Bupe Mwakang’ata akishukuru baada ya kupokea msaada wa mifuko 200 ya
saruji yenye thamani ya shilingi 3.7 kutoka benki ya TPB. Mifuko hiyo itakwenda
kusaidia ukamilishaji wa ujenzi wa madarasa ya shule mbalimbali Mkoani hapo.
Kulia ni Mkurugenzi wa Teknohama na Uendeshaji wa benki ya TPB Jema Msuya, na
kushoto ni Meneja wa benki ya TPB tawi la Sumbawanga Damas Joseph. Hafla hiyo
fupi ya makabidhiano ilifanyika kwenye ofisi za CCM Mkoa wa Rukwa.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa
Rukwa Reiner Rukalah (katikati) akizungumza mara baada ya kupokea msaada
wa mifuko 200 ya saruji yenye thamani ya
shilingi milioni 3.7 kutoka kwa benki ya TPB. Mifuko hiyo itakwenda kusaidia
ukamilishaji wa ujenzi wa madarasa ya shule mbalimbali Mkoani hapo. Kushoto ni
Mbunge wa Viti Maalum wa Rukwa Bupe Mwakang’ata na kulia ni Meneja wa benki ya
TPB tawi la Sumbawanga Damas Joseph. Hafla hiyo fupi ya makabidhiano ilifanyika
kwenye ofisi za CCM Mkoa wa Rukwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...