Rasmi, kutokana na kuepuka maambukizi ya Virusi vya Corona, Ligi mbalimbali duniani zimesimamishwa.
Vyama vya soka katika nchi hizo zimetangaza kusimamisha michezo kadhaa hadi mwezi wa Aprili.
Ligi kuu ya Uingereza (EPL) imetangaza kusimamisha michezo yote ya mpira wa miguu, FA, Premier League, EFL na Barclays FA Women’s Super League, pamoja na FA Women’s Championship hadi Aprili 04 mwaka huu ili kuepuka maambukizi ya virusi hivyo.
Ligi kuu Ufaransa (Ligue 1) pamoja na Ligue 2 zimesimamishwa kutokana na kuhofia maambukizi ya virusi vya CORONA.
Ligi kuu Ujerumani kuanzia Machi 17, michezo yote itasimama kwa muda hadi April 2, ili kuepuka maambukizi ya virusi vya Corona ila kwa wikiendi hii mechi zitachezwa bila kuwa na mashabiki.
Hadi sasa, Michezo ya Klabu Bingwa Ulaya na Ile ye Europa League imehairishwa kwa muda ikiwemo na Ligi ya Italia ambapo awali walikuwa wanacheza bila mashabiki.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...