Na Said Mwishehe, Michuzi TV

MAGARI ya usafiri maarufu kwa jina la Daladala leo yameanza kubeba abiri kwa idadi ya viti 'Level Seat' ikiwa ni mkakati wa kupambana na  kuenea kwa virusi vya  Corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19.

Utaratibu huo umeanza leo Machi 31 mwaka huu wa 2020 na hivyo kwenye vituo mbalimbali vya daladala mamia ya abiria ya wakazi wa Jiji hilo wameonekana wakiwa kituoni kwani daladala nyingi zilikuwa zikifika vituoni yakiwa yameshajaa abiria kutokana na utaratibu huo.

Mwandishi wa Michuzi Blogu na Michuzi TV  leo imetembelea vituo mbalimbali vya daladala na kushuhudia idadi kubwa ya watu wakisubiria usafiri wa daladala.Hata hivyo wale ambao wanapanda daladala hizo mwanzo wa kituo wamekuwa na uhakika mkubwa wa kupata kiti lakini wale wa katikati ya vituo wamekuwa na changamoto kubwa ya kupata gari.

Mkazi wa Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam Ziberi Mwinyigoha amesema utaratibu huo wa kukaa kwenye viti ni mzuri lakini changamoto kubwa muda mwingi watu wamekuwa vituoni kwani magari yanajaa haraka tofauti na ilivyokuwa awali.

" Kwa hapa kituo cha Gongo la Mboto changamoto kubwa iliyopo.daladala nyingi zinakuja zikiwa nimejaa kwani zinabeba abiria kuanzia Banana na kisha kufanya hivyo hadi likifika Kituo  Kipya kunakuwa hakuna nafasi ya kukaa na matokeo yake tumejikuta hatuna cha kufanya. Nadhan kuna haja ya Serikali kukaaa na wadau wa usafiri kuangalia namna  ya kuondoa changamoto hii," amesema Mwinyigoha.

Mkazi wa Tabata Asha Shabani amesema kwenye daladala za upande wao watu wengi sana walikuwa wakihaha kitafuta usafiri na baadhi ya abiria wengine wanalazimisha kuingia kwa kukaa chini ili wasionekana kama wamesimama.

Shaban amefafanua kuwa akiwa akiwa ndani ya daladala linalotoka Kimanga kwenda Mnazi Mmoja aliwasikia kondakta na dereva wake wakishauriana kesho waweke benji kwa ajili ya abiria kukaa.Hata hivyo ushauri ulisababisha baadhi ya abiria kuanza kucheka na wengine kuunga mkono.

Mkazi wa Segerea jijini Dar es Salaam John Mwantone amesema wanailewa nia njema ya Serikali katika kupambana na Corona lakini ni vema utaratibu huo ukaendelea kuboreshwa ili kuhakikisha changamoto ambayo imeonekana leo inaondolewa.

Wakati huo huo  Goga jijini Dar es Salaam ,imeelzwa hali ya usafiri ilikuwa shwari na watu wanafuata  utaratibu ambao ulikuwa unatolewa na makondakta wa daladala.Juma Kindamba ambaye anaishi Goba amesema kuwa kwake anapongeza utaratibu wa abiria kukaa badala ya Kusimama kwani kusimama kwenye daladala kuambukizana Corona inakuwa rahisi.

Hata hivyo changamoto kubwa imeonekana kwenye bei kwani kuna baadhi ya daladala ambazo zilizokuwa zinabeba abiria waliokuwa wanazunguka na gari walikuwa wanatoza Sh.1500 na baadhi ya daladala hizo ni zile zinazofanya safari kati ya Kivukoni na Gongo la Mboto.

Kwa upande wa madereva na makondakta nao wametoa maoni yao baada ya leo kuanza  kubeba abiria kwa utaratibu wa level Seat ambapo wameeleza ni utaratibu mzuri lakini umekuwa wa maumivu kwa upande wao.

Dereva wa daladala ya  Posta Mpya Makumbusho aliyejitambulisha kwa jina  Adolf amesema wanatambua kuna Corona na Serikali inachukua tahadhari zote za kukabiliana na ugonjwa huo lakini ukweli wao wako kwenye wakati mgumu.

Amefafanua kuwa  wamiliki wa daladala hawana tatizo kwani angalua wamepunguza kiasi cha fedha akitoa mfano yeye hesabu kwa tajiri kwa siku ni Sh.80,000 lakini baada ya utaratibu huo anatakiwa kupeleka Sh.60,000.

"Kwa tajiri hakuna tatizo lakini kazi iko kwenye mafuta kwani bado tunakwenda safari zile zile  na tunaanza mafuta kwa bei iliyopo sasa,hivyo kwenye mafuta ndiko ambako kunatufanya sisi madereva na abiria tukose fedha kabisa.Tumekuwa watu wa kutafuta hela ya tajiri na mafuta tu.Hivyo ushauri wangu iko haja kwa Serikali kuangalia kwenye eneo la mafuta,"amesema.

Kwa upande wake  Kondakta wa gari ya Makumbusho - Posta Mpya Eliasi Aman amesema kuwa ni kweli Serikali inataka kuona watu wake wanakuwa salama lakini kwa upande wao wa madereva na makondakta hali yao kiuchumi itakuwa ngumu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...