Na Ahmed Mahmoud,Arusha
Serikali imewahakikishia wamachinga kuendelea kufanyabiashara kwenye soko la Samunge lililoungua moto na kuwaondolea hofu iliyojengeka kwamba ina mpango wa kuwaondoa katika soko hilo.

Akiongea na maelfu ya wafanyabiashara hao zaidi ya 5000 Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro ameigiza halmashauri ya jiji la Arusha kuhakikisha wanaharakisha kujenga miundombinu ya soko hilo ili kuwapa nafasi wafanyabiashara kuendelea na shughuli zao.

Ameeleza kuwa hakuna mfanyabiashara mdogo aliyekuwa anafanyabiashara katika soko hilo atakayeondolewa bali serikali inahitaji kuweka sawa hali ya ufanyaji wa biashara ndani ya soko hilo.

"Niwatoe hofu hakuna mtu atakayeondolewa ndani ya soko hilo kama maneno yanavyopita chini chini msiyasikilize kwa kuwa serikali inahitaji kuweka mazingira rafiki ya ufanyaji wa biashara ndani ya siku saba itakuwa teyari"Amesema Daqarro

Amebainisha kuwa halmashauri itaendelea  kufanya tathmini ya miundombinu rafiki kwa majanga ili kuondoa changamoto iliyojitokea wakati wa kuzima moto ikiwemo kuweka nafasi za kuweza kupitika ndani ya soko hilo.

Katika hatua nyingine Daqarro ameagiza kufungwa kwa barabara mojawapo iliyo kando ya soko hilo ilikutoa fursa kwa baadhi ya wafanyabiashara ambao bidhaa zao hazikuunguliwa na moto kuendelea na biashara zao hadi miundombinu ya soko hilo itakapokuwa tiyari.

Hata hivyo aliwataka wafanyabiashara waliounguliwa kufanya usafi na kutoa mabaki ya mabati ili kupisha soko hilo kufanyiwa marekebisho, tathmini na miundo mbinu .

Awali aliyekuwa mstahiki meya wa jiji la Arusha Kalist Lazaro ametoa pole kwa wafanyabiashara hao huku akipongeza uamuzi wa serikali kwa kuruhusu wafanyabiashara hao wadogo kuendelea na shughuli zao katika soko hilo mara baada ya marekebisho kukamilika.

Naye Mwenyekiti wa wamachinga Mkoa wa Arusha Amina Njoka ameishukuru serikali kwa hatua kuweza kuwaruhusu kuendelea kufanya biashara katika soko hilo kwani walikuwa gizani hawajui hatma yao ambapo alitoa angalizo kwa serikali kuendelea kuwasimamia ili kila moja aweze kupata eneo lake la biashara na kuondoa wavamizi.

Sehemu ya bidhaa ziliongua ndani ya soko la machinga la Samunge lililoungua usiku wa kuamkia Jana jijini Arusha ambapo Serikali imefunga barabara moja ili wafanyabiashara hao kuendelea na kazi zao picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha.
Mabaki ya mabati baada ya kuungua kwa soko la machinga Samunge Jiji Arusha usiku wa kuamkia Jana
Sehemu ya bidhaa zizonusurika kuungua Moto ndani ya soko la machinga Samunge jijini Arusha.

Muonekano wa eneo la soko la Samunge baada ya kuungua Moto usiku wa kuamkia Jana jijini Arusha
Hali ilivyokuwa leo Mara baada ya Moto kuzima ambapo wafanyabiashara wameruhusiwa Leo kufanya Usafi na kuondoa mabaki hayo.
Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Arusha wakipita kukagua sehemu mbali mbali na baadae kuongea na wafanyabiashara hao

Ndio hali halisi inavyoonekana Mara baada ya kuungua kwa Moto Soko la Samunge
Kamati ya Ulinzi ya wilaya ikipita kukagua maeneo yalioathirika na Moto ulioteketeza Soko la Machinga jijini Arusha picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...