Kikundi cha Wanawake na Mabadiliko Manispaa ya Shinyanga (Women For Change - WFC) kimekabidhi bweni walilokarabati kwenye kituo cha kulea watoto wenye ulemavu mbalimbali cha Buhangija Jumuishi, wakiwamo na watoto wenye ualbino kwa ajili ya kuwaweka katika mazingira mazuri. Zoezi la kukabidhi bweni ambalo ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, limefanyika leo Alhamis Machi 5, 2020 ambapo mgeni Rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, huku hafla hiyo fupi ikihudhuriwa pia na maofisa elimu, pamoja na wajumbe wa kamati ya shule ya msingi Buhangija.


Akizungumza wakati wa kukabidhi bweni hilo, Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, amekipongeza Kikundi hicho cha Wanawake na Mabadiliko Manispaa ya Shinyanga kwa moyo wa kujitolea kulifanyia ukarabati bweni moja la wavulana ambalo lilikuwa limechakaa miundombinu yake, na hatimaye watoto hao wataishi kwenye mazingira mazuri.


Amesema jukumu la kulea watoto hao wakiwamo wenye ualbino ni la kila mtu na siyo kuiachia Serikali peke yake kuwatunza, ambapo jamii pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo kutoka ndani ya mkoa wa Shinyanga na nje, wanapaswa kuwa hudumia ili kutatua changamoto zinazowakabili. “Serikali inakipongeza chama hiki cha Wanawake na Mabadiliko kwa kujitolea kufanya ukarabati wa bweni hili moja la wavulana kwenye kituo cha buhangija cha kulea watoto wenye ulemavu mbalimbali wakiwamo wenye ualbino, ili waishi katika mazingira mazuri,”amesema Mboneko.


“Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili watoto hawa, ikiwamo upungufu wa walimu maalumu, ukarabati wa miundombinu, pamoja na ujenzi wa uzio kwenye majengo mapya ili kuimarisha ulinzi,”ameongeza.


Naye katibu wa Kikundi cha Wanawake na Mabadiliko Manispaa ya Shinyanga (Women For Change - WFC), Lucy Mwita, amesema katika kuelekea kwenye kongamano lao la siku ya wanawake duniani, ambalo watalifanya siku ya Jumamosi,Machi 7,2020 wameona kabla ya tukio hilo ni vyema wafanye kitu kama wanawake, na kuamua kukarabati bweni hilo.


Mwita ametoa wito kwa uongozi wa kituo hicho kulitunza bweni hilo ambalo limegharimu kiasi cha Shilingi 2,450,000/= ili lidumu kwa muda mrefu na kutunza watoto hao katika mazingira mazuri, huku wakigawa zawadi ya juisi, na biskuti.


Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule ya msingi Buhangija na mlezi mkuu wa kituo hicho cha watoto wenye ulemavu mbalimbali wakiwamo wenye ualbino Seleman Kipanya, ameshukuru chama hicho kwa kukarabati bweni hilo, huku akiomba wadau wengine wajitokeze kufanya ukarabati mabweni yaliyosalia ili kuwaweka watoto hao katika mazingira mazuri ya kuishi.

Kikundi cha Wanawake na Mabadiliko Manispaa ya Shinyanga (Women For Change - WFC), kinajihusisha na Ununuzi wa Hisa ili kuinuana kiuchumi na chenye mfuko wa kusaidia jamii na watoto walioko kwenye mazingira magumu. Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye kituo cha kulea watoto wenye ulemavu mbalimbali wakiwamo wenye ualbino wanaolelewa Buhangija wakati Kikundi cha Wanawake na Mabadiliko Manispaa ya Shinyanga (Women For Change - WFC) kikikabidihi bweni kilichokarabati leo Machi 5,2020 ambapo alisema Serikali kwa kushirikiana na wadau wataendelea kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye hafla hiyo ya kukabidhi bweni lililokarabatiwa na Kikundi cha Wanawake na Mabadiliko Manispaa ya Shinyanga (Women For Change - WFC) na kuwapongeza kwa kazi hiyo nzuri ambayo wameifanya. Katibu wa Kikundi cha Wanawake na Mabadiliko Manispaa ya Shinyanga (Women For Change - WFC) Lucy Mwita akisoma taarifa ya chama hicho namna walivyoguswa kukarabati bweni moja la wavulana kwenye kituo hicho cha watoto Buhangija. Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Buhangija na mlezi mkuu wa kituo hicho cha watoto Buhangija Selemani Kipanya akisoma taarifa ya kituo hicho na kupongeza Kikundi cha Wanawake na Mabadiliko Manispaa ya Shinyanga (Women For Change - WFC) kwa kufanya ukarabati wa bweni moja la wavulana. Afisa Elimu wa shule za msingi manispaa ya Shinyanga Neema Mkanga, akizungumza kwenye hafla hiyo fupi ya kukabidhi bweni hilo. Watoto wenye ualbino wakiwa kwenye hafla ya kukabidhiwa bweni lililokarabatiwa na Kikundi cha Wanawake na Mabadiliko Manispaa ya Shinyanga (Women For Change - WFC). Mtoto mwenye ualbino Rajabu Yahaya akitoa shukrani kwa kukarabatiwa bweni lao na kuishi kwenye mazingira mazuri. Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko (kulia), akikata utepe ili kufungua bweni la wavulana kwenye kituo cha kulea watoto wenye ulemavu mbalimbali wakiwamo wenye ualbino, akiwa na wajumbe wa Kikundi cha Wanawake na Mabadiliko Manispaa ya Shinyanga (Women For Change - WFC) ambao ndiyo wamelifanyia ukarabati bweni hilo. Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko kulia akikagua ukarabati wa bweni hilo la wavulana, akiwa na mwalimu na mlezi mkuu wa kituo hicho cha Buhangija Selemani Kipanya. Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko kulia akikagua ukarabati wa bweni hilo la wavulana katika kituo cha Buhangija. Wajumbe wa Kikundi cha Wanawake na Mabadiliko Manispaa ya Shinyanga (Women For Change - WFC) wakigawa juisi na biskuti kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija. Wajumbe wa Kikundi cha Wanawake na Mabadiliko Manispaa ya Shinyanga (Women For Change - WFC) wakigawa juisi kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija. Wajumbe wa Kikundi cha Wanawake na Mabadiliko Manispaa ya Shinyanga (Women For Change - WFC) wakigawa juisi na biskuti kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija. Awali mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akisalimiana wajumbe wa chama cha wanawake Shinyanga mjini (Women For Change) wakati alipowasili kwenye kituo hicho cha kulea watoto Buhangija na kutekeleza ushauri wa Waziri wa Afya Ummy Mwalimu wa kusalimina bila ya kushikana mikono ili kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona. Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiwa na Wajumbe wa Kikundi cha Wanawake na Mabadiliko Manispaa ya Shinyanga (Women For Change - WFC) , pamoja na watoto wenye ualbino wakipiga picha ya pamoja. Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiwa na Wajumbe wa Kikundi cha Wanawake na Mabadiliko Manispaa ya Shinyanga (Women For Change - WFC) pamoja na watoto wenye ualbino wakipiga picha ya pamoja mbele ya bweni ambalo limekalabatiwa na wanawake hao. Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akipiga picha ya pamoja naWajumbe wa Kikundi cha Wanawake na Mabadiliko Manispaa ya Shinyanga (Women For Change - WFC) mbele ya bweni ambalo wamelikarabati. Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...