Na Amiri Kilagalila, Njombe

Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri amesema watanzania wataendelea kuungana katika mapambano dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa Corona (COVID-19) na kamwe hawawezi kuacha ugonjwa huo ukatawala.

Ruth Msafiri ameyasema hayo wakati akiahirisha ibada ya kufunga na kuombea maambukizi ya virusi vya COVID-19 iliyofanyika kwa wiki moja na waumini wa kanisa la Tanzania assemblies of God (T.A.G) Melinze lililopo halmashauri ya mji wa Njombe mkoani humo.

“Corona imeingia Duniani na imekanyaga Tanzania lakini kwa kumwamini Mungu wetu aliye hai,wakati tunapombana na Corona tutayaunganisha na magonjwa mengine kwasababu ni utumishi wa shetani,Corona hatutaweza kumwacha akatawala,hatutampa ufalme amekuja kwa njia moja kwa njia saba lazima atawanyike tuombeni bila kuchoka”alisema Ruth Msafiri

Vile vile Msafiri amesema pamoja Mungu kusikia dua,imani na sala za wanadamu wanao lia juu ya gonjwa hilo,ametoa rai kwa watanzani kuendelea kuchukua tahadhari kubwa juu ya COVID-19.

“Naimani Mungu ameskia sala zetu,lakini niwaombe wenzangu pamoja na imani tuliyonayo,tuchukue tahadhari kwa kunawa mikono kila wakati,tusipeane mikono,tusikumbatiane na tuepuke mikusanyiko yoyote isiyokuwa ya lazima kwa kipindi maalumu ambacho tunaamini ndani ya siku 30 hizi tunaamini hili gonjwa litakuwa limepotea mbali,tukifanya hivyo tutapona”aliongeza Msafiri

Naye mchungaji kiongozi wa kanisa la T.A.G Melinze, Sefania Tweve amesema kwa kuona umuhimu wa kuombea janga hilo,waumini wa kanisa wameungana kwa ajili ya kufunga na kuomba na kwa sasa wanaamini Mungu atamaliza ugonjwa wa COVID-19

“Na tumekuwa na maombi ya mara kadhaa tukiombea Corona,familia na uchumi wa nchi kwa kuwa la kwanza tunataka Mungu aiponye nchi yetu,na mategemo yetu tumemuomba bwana kwa kuwa sasa tunajua atamaliza Corona na ataponya magonjwa”alisema Mchungaji Tweve

Baadhi ya waumini wa kanisa hilo akiwemo Anna Mayemba na Marko Chengula wamekiri kwasasa kuwa maambukizi ya COVID-19 ni tishio,ndio maana kanisa hilo limeona uzito wa kufanya maombi.

“Sasa kama kanisa tumeamua kuwa na maombi rasmi kwa ajili ya kupambana dhidi ya Corona,na kama kanisa tumeamua kufanya hivi ili listufikie na kuungana na serikali yetu katika kukemea janga hili”alisema Marko Chengula

Waumini wa kanisa hilo wameingia katika maombi ya kufunga na kuomba kwa ajili ya maradhi ya Corona,kuombea nchi,kukemea roho ya magonjwa,uchumi pamoja na familia.

Aidha mpaka sasa kwa mujibu wa taarifa ya serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania iliyotolewa na waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto,idadi ya  wagonjwa  imeongezeka kutoka 13 na kufikia 19 waliogundulika kuwa na maambukizi ya virusi vya COVID-19,wakati huo mgonjwa wa kwanza kugundulika na maambukizi hayo akiwa amepona na wengine wakiendela vizuri.
 Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri akizungumza na waumini wa kanisa la T.A.G Melinze mjini Njombe wakati akifunga maombezi ya wiki moja dhidi ya Corona yaliyofanya na kanisa hilo.
  Baadhi ya waumini wa kanisa la T.A.G wakiendelea na ibada ya maombezi.
 Mchungaji wa kanisa la T.A.G Sefania Tweve akizungumza baada ya ibada namna kanisa lilivyoingia katika maombezi ili kuombea taifa.
Sehemu ya kanisa la T.A.G Melinze lililopo mtaa wa Melinze mjini Njombe

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...