Waziri wa Fedha na Mipango,Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), amewateua
wajumbe wawili watakaoiwakilisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye
Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Madini ya Twiga (Twiga Minerals Corporation Limited).
Wajumbe walioteuliwa ni
1.
Bw. Casmir Sumba Kyuki
2.
Bw. Michael Jonathan
Kambi
Uteuzi wa wajumbe hao watakaotumikia nafasi zao kwa kipindi cha miaka
mitatu, unafuatia makubaliano mapya ya namna ya kuendesha Kampuni hiyo kwa ubia,
yaliyofikiwa kati ya Serikali na Kampuni ya Barrick Gold, na kutiwa saini tarehe
24 Januari, 2020, Jijini Dar Es Salaam.
Kampuni ya Madini ya Twiga inasimamia migodi mitatu ya Buzwagi, North
Mara na Bulyanhulu ambapo Barrick Gold inamiliki asilimia 84 ya hisa na Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inamiliki hisa asilimia 16.
Uteuzi wa wajumbe hao unaanza
leo tarehe 22 Machi 2020
Imetolewa na:
Benny Mwaipaja
Mkuu wa Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na
Mipango
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...