Na Karama Kenyunko, Michuzi Globu ya Jamii.

MKURUGENZI Mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga amewasilisha maombi katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi ( Mahakama ya Mafisadi), ya kuomba kutaifishwa kwa akaunti mbili za USD na moja ya EURO zenye jumla ya Shilingi bilioni 16.7 za upatu kuwa mali ya Serikali kutokana na washtakiwa hao raia wa kigeni kutofika mahakamani
Washtakiwa hao ni  raia wa Ujerumani Manon Huebenthal na raia wa Uingereza Frank Ricket ambapo wanashtakiwa na kampuni yao ya IMS Maketing Tanzania Ltd.

Imedaiwa Februari 11, 2019 DPP aliwafungulia washtakiwa hao mashtaka matatu ya kula njama, kuendesha shughuli za upatu na kutakatisha fedha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu lakini hata hivyo washtakiwa hawakuwahi kufika mahakamani.

Kutokana na kutokufika kwao, Machi 15, mwaka 2019 Mahakama ilitoa amri ya kukamatwa kwa washtakiwa hao lakini pia hawakuweza kupatikana. Kwa mazingira hayo DPP aliwasilisha maombi katika Mahakama hiyo ya mafisadi akiomba fedha hizo zitaifishwe na kuwa mali ya Serikali, ambapo katika maombi hayo yaliyosikilzwa leo Machi 30,mwaka 2020 na Jaji Elinaza Luvanda wa Mahakama imepanga kutoa uamuzi wa maombi hayo, Aprili 3,mwaka 2020.

Maombi hayo yameungwa mikono na kiapo cha Wakili wa Serikali, Estazia Wilson pamoja na kiapo cha SSP Fadhili (Mpelelezi ), ambapo upande wa Jamhuri katika kesi hiyo leo umewakilishwa na DPP, Wakili wa Serikali Mkuu, Shadrack Kimaro na Wakili wa Serikali Mkuu, Christopher Msigwa.

Imeelezwa  washtakiwa hao walikuja nchini Tanzania  na kuanzisha Kampuni ya IMS Marketing Tanzania Ltd, Novemba 19,2014 na kupewa usajili wa namba 113133, ambapo Huebenthal na Ricket ni Wakurugenzi na pia wanahisa katika Kampuni hiyo lakini kuendesha upatu haikuwa shughuli ya Kampuni hiyo poa katika kipindi hicho.

Washtakiwa hao wanadaiwa kuanza kusaini nyaraka mbalimbali kwa mawakili kwa ajili ya hiyo kampuni na kwamba  Aprili 23, 2015 walifungua akaunti mbili za USD katika Benki ya Afrika (BOA), Tawi la NDC lililopo jijini Dar es Salaam  kwa jina la Kampuni ya IMS.
Aidha Mei 3, 2016 washtakiwa hao walifungua akaunti ya EURO mbapo kwa kipindi hicho walipata leseni ya biashara kutoka Manispaa ya Kinondoni kwa ajili ya kufanya shughuli za Masoko katika manispaa hiyo.

Imeendelea kuelezwa kuwa  Kampuni hiyo ya IMS Marketing ina mahusiano na Kampuni ya IMS international Marketing Services ambayo imesajiliwa na inafanya shughuli zake nchini Singapore, pia Kampuni hizo mbili zinauhusiano wa karibu na ni sehemu ya Kampuni nyingine inayoitwa One Coin Ltd ambayo ilianzishwa Aprili, mwaka 2014 huko Gibraltar.

DPP ameendelea kueleza kuwa kampuni hiyo ina ofisi zake nchini Bulgaria, Falme za Kiarabu na Hong Kong, ambapo  inajihusisha na masula ya upatu pamoja na kampuni zingine, ambapo ni kosa tangulizi la utakatishaji fedha, pia kampuni hiyo ya One Coin, katika maneno mbalimbali ya nje ya nchi ilizuiliwa kufanya shughuli za upatu na akaunti zake za benki zilizoingizwa fedha zilikamatwa, baada ya hapo kwenye mitandao yao ya kijamii waliwataka wanachama wao kuendelea kutoa michango yao kupitia akaunti za BOA benki.

Imeadaiwa kuwa kwa nyakati tofauti tofauti, akaunti hizo zilipokea USD 1,337,965.90 na nyingine dola za Marekani  15,631.97 huku akaunti ya Euro ikipokea Euro 5,442,020.5 ili kuonesha mahusiano kati ya washtakiwa hao miamala ilianza kufanyika kwa Huebenthal,  Ricket na Kampuni ya IMS International.

Pia imedaiwa kati ya Novemba 18,mwaka 2015 na Juni 31, mwaka 2016, Dola za Marekani 61,643.84 zililipwa kwa IMS International huku kati ya Juni  31,2016 na Novemba mwaka 2016 dola za Marekani 29,549.7 zililipwa kwa mshtakiwa Ricket na Euro 19,195.75 zilihamishiwa kwa mshtakiwa Ricket ambapo kwa ujumla kwenye akaunti hizo,  akaunti moja ya dola za Marekani  ilikuwa na 1,337,965.90 na ya pili ilikuwa  na kiasi cha dola 13,631.89 huku kwenye akaunti ya Euro kulikuwa na 5,377,306.50.
Kutokana na uzito wa ushahidi unaonesha miamala hiyo ilisababisha DPP kufungua mashtaka dhidi ya washtakiwa hao na badae aliwasilisha maombi katika Mahakama ya Kisutu kuzuia uendeshaji wa hizo akaunti.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...