Na Jusline Marco-Arusha

Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limewataka wananchi kutoa taarifa haraka kwa Jeshi la Polisi na Jeshi la zima moto na uokoaji pindi wanapoona majanga ya moto yanapotokea ili kuweza kuyadhibiti kwa haraka kabla hayajaleta madhara makubwa.

Akitoa taarifa za kutokea kwa tukio hilo  kwa waandishi wa habari Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani humo KOKA MOITA ACP amesema tukio hilo limetokea jana majira ya saa tano na nusu usiku katika Soko la Samunge lililopo Mtaa wa NMC,Kata ya Kati,Tarafa ya Themi(Temi) Halmashauri ya Jiji la Arusha ambapo moto huo bado chanzo chake hakijafahamika.

Kamanda Moita amesema kuwa moto huo umeweza kuteketeza vibanda katika soko hilo ambavyo vimejengwa kwa mabati,mbao na mabanzi huku idadi kamili na tathimini yake bado haijafahamika.

Aidha Kamanda Moita amesema kuwa wakati zoezi la uzimaji wa moto huo likiendelea mtu mmoja mkazi wa Moshono jijini Arusha aliyefahamika kwa majina ya James Peter Temba mwenye umri wa miaka 57 mchanga,mkristo mfanyabiashara ambaye ni mmoja kati ya wamiliki wa vibanda vilivyoungua ndani ya soko hilo amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu kwenye Hospitali ya rufaa ya mount meru kutikana na mshituko alioupata baada ya kufika katika eneo la tukio na kukukuta kibanda chake kikiteketea kwa moto.

Aidha amsema kuwa uchunguzi bado unaendelea ili kubaini thamani halisi ya mali zilizoungua pamoja na kujua chanzo cha moto huo ambapo mwili wa marehemu huyo umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya mount meru kwa uchunguzi zaidi.

Naye Mkuu wa Wialaya ya Arusha Gabriel Daqarro katika tukio hilo amewapa pole wafanyabiashara waliokutwa na janga hilo ambapo amesema kuwa kwa sasa zoezi linaloendelea ni utambuzi wa wamiliki halali wa vibanda vilivyoungua na wale wenye vibanda ambavyo moto haujafika ili kuweza kurahisisha kazi ya ufanyaji wa tathimini ya mali hizo kupitia wataalamu.

"Ninachowaomba wananchi na qafanyabiashara wa jiji la Arusha watulie wakati serikali inaendelea kufanya uchunguzi wa jambo hili kwa upande wa vyombo vya dolla lakini kwa upande wa wathamini ili tuweze kujua hasara ili iliyopatikana halisi ni shilingi ngapi,vibanda vingapi,watu wangapi.Alisema Daqarro

Vilevile ameongeza kuwa katika soko hilo upande wa ndani kulikuwa na vibanda zaidi ya elfu 3 na kwa mzunguko wa nje ni vibanda zaidi ya elfu 6 ambapo idadi hiyo imetokana na soko hilo kuwa ni soko ka kimachinga.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Bwn.Agney Chitukuro amesema kuwa kama serikali ya mkoa jukumu lao ni kufanyatathimini ya hasara ya mabanda yaliyoungua na mali zilizoteketea na kupeleka taarifa hizo katika ofisi ya waziri mkuu kitengo cha maafa ili waweze kutoa maelekezo.

Amebainisha kwa kutoa pole kwa wafanyabiashara waliopoteza mali zao na kusema soko hilo lilikuwa likiwasaidia katika kujiingizia kipato sambamba na wananchi kupata bidhaa mbalimbali.

Mabaki ya vibanda vya wafanyabiashara vilivyoteketea kwa moto katika soko la Samunge,Jijini Arusha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...