Na Said Mwishehe,Michuzi Globu ya jamii

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema linawashikilia watu wawili ambao ni mume na mke kwa tuhuma na kueneza taarifa za uongo kwa wananchi kuhusu ugonjwa COVID-19(Corona) na kwamba watafikishwa mahakamani wakati wowote.

Akizungumza leo  Machi 27 mwaka 2020 ,Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amesema watu hao wamekamatwa Machi 20 mwaka huu saa saba mchana  wakiwa kwenye daladala aina ya Toyota DCM namba T 119 DKS iliyokuwa ikitokea Muhimbili.

Amewataja watu hao ni Boniphace Mwita na mkewe Rosemary  Mwita Mwita kwamba wakiwa kwenye daladala hiyo walianza kupotosha na kutoa kejeli kwa umma kuwa hakuna nchini kwetu hakuna Corona ila Serikali inasema hivyo kwasababu haina fedha na ndio maana imefunga shule kwani wamekosa hela za chakula cha wanafunzi.

Kamanda Mambosasa amesema kuwa kutokana na kejeli na uzushi wa watu hao abiria waliokuwepo ndani ya daladala hiyo walikasirishwa na kuchukua hatua za kuwaweka chini ya ulinzi na  kuitaka daladala hiyo ipelekwe Kituo cha Polisi na sasa wanashikiliwa na jeshi hilo kwa ajili ya hatua inayofuata ya kuwapeleka mahakamani.

Amesisitiza kuwa Jeshi la Polisi limeshachukua maelezo ya watuhumiwa hao na jarada tayari wameshapeleka law Wakili wa Serikali kwa ajili ya hatua nyingine za kisheria.

Kamanda Mambosasa ametoa rai kwa Watanzania kutotoa taarifa za kejeli na dhihaka kuhusu ugonjwa wa Corona na kwamba jeshi hilo halitasita kuchukua hatua kwa watakaobainika wanafanya upotoshaji.

"   Wenye tabia ya kupotosha kuhusu ugonjwa huu wa Corona waache mara moja, tunashauri wananchi kuendelea kufuata maelekezo yanayotolewa na viongozi wa Serikali pamoja na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto na si vinginevyo,"amesisitiza Kamanda Mambosasa.
 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa  akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, baada ya kukamata vitu mbaimbali zikiwepo Kompyuta mpakato,Risasi  na bunduki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...