Na Said Said Mwishehe, Michuzi Globu ya jamii

KADRI muda unavyosonga mbele kuelekea mechi ya watani wa jadi Yanga na Simba itakayochezwa leo Machi 8 mwaka huu 2020, saa 11 jioni mashabiki lukuki wameanza kujitokeza katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam huku kila upande ukiwa umejawa na tambo za ushindi.

Mechi ya Yanga na Simba ni moja ya mechi ambazo zimekuwa na utamaduni mkubwa wa kujaza mashabiki, wapenzi na wachama wa vilabu hivyo hasa kwa kuzingatia ni mechi ambayo hutawaliwa na kila aina ya mbwembwe nyingi ambazo mwisho wa siku dakika 90 za mchezo huamua nani mbabe dhidi ya mwingine.

Yanga katika mchezo wa leo ndio mwenyeji  na viingilio vya mchezo huo ambapo na maelfu wa mashabiki wa soko akiwemo mgeni rasmi  Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika CUF Ahmad Ahmad ambapo bei ya viingilio ni kuanzia Sh.7000, 10000, 20000 na 30,000
 Kwa kukumbusha tu mchezo uliopita wa watani wa jadi, walitoka sare ya mabao 2-2 na leo huenda mchezo utaamua nani atamfunga mwenzake au wataendeleza sare kwa mara nyingine. Yanga wamekuwa wakitamba kuwa mchezo wa leo lazima wataibuka na ushindi hasa kutokana na kuimarika kwa Kikosi chao huku jicho la Wanayanga wengi likielezwa kwa mchezaji wao aliyesajiliwa kipindi cha dirisha dogo la usajili Bernard Morrson na hasa baada ya kuonesha umahiri wake wa kusakata soka tangu ajiunge na Yanga.

Pia wana Yanga wamekuwa wakijivunia uwepo wa David Mollinga, Detrim  Nchimbi, Papii Shishimbi, Haruna Niyonzima, Mapinduzi Balama na wengine wengi huku katika lango lao akiwa Metacha Mnata .

 Wakati Simba wao wanayojivunia ubora na umahiri wa Kikosi chao huku mchezaji  Luis Miqueson a.k.a Konde Boy, Clatus Chota Chama, Fransis Kahata, Deo Kanda, Medie Kagere, Hassan Dilunga HD, John Bocco,  Abdulrahman Shariff Shibob, Pascal Wawa ,Mohamed Husaein Zimbwe a.k.a Shabalala pamoja na wachezaji wengine wanapenda Kikosi cha timu yao huku golini kukiwa na Aish Salum Manulla.

Hata hivyo pamoja na tambo hizo historia inaonyesha kuazia mwaka 2000 hadi mwaka 2020 Simba imeifunga Yanga mara 14, Yanga wameshinda mara sita na sare 21.Pamoja na rekodi hiyo ya historia ya watani wa jadi bado wanapokutana huwa na shughuli pevu.

Cha kukumbuka tu ni kwamba kwa ujumla Yanga ambayo ni bingwa wa kihistoria kwa rekodi za jumla za Ligi ya Tanzania Bara Yanga wamechukua Kombe mara 27 na Simba mara 20.

Kwa sasa Simba anaongoza Ligi kwa alama 68 wakati Yanga ana alama 47 na hivyo Yanga inashika nafasi ya nne huku nafasi ya kwanza ikishikiliwa na Simba ,Azam nafasi ya pili akiwa na alama 51, nafasi ya tatu Namungo FC mwenye alama 48.

 Hata hivyo ikiwa imetimia saa saba mchana mashabiki wa Simba wameonekana kuja mapema kwenye Uwanja wa Taifa kwani upande wao tayari nusu ya eneo limejazwa wakati upande wa Yanga ukiwa bado  mweupe ukiondoa sehemu ndogo.Kwa kuwa mechi ni saa 11 jioni huenda kila upande ukawa na idadi sawa ya mashabiki kwani Simba na Yanga mbali ya matokeo ya uwanjani ,kujaza Uwanja nako kumekuwa na sifa ya kujivunia.

Itoshe kueleza kuwa dakika 90 za.mchezao wa Simba na Yanga ndizo zitaamua nani mbabe .Hivyo mashabiki na wapenzi wa soka macho na masikio yao kwa leo ni Uwanja wa Taifa.Kila laheri Yanga,kila laheri Simba.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...