Na Mwandishi Wetu,Michuzi Globu ya jamii

KATIKA kuelekea Siku ya Data wazi Duniani, Asasi ya Kituo cha Habari, Amani na Usalama Barani Afrika(CIPSA) umetoa mwito kwa raia kuendelea utamaduni wa kufuatilia habari sahihi na uwazi ili kuwasaidia katika kusukuma maendeleo yao ya kibinafsi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo hii katika kile alichokiita wiki ya uhamasishaji kupata habari sahihi kuhusu maendeleo yao kuelekea kilele cha siku ya data wazi duniani Machi 7 mwaka huu, Mkurugenzi wa CIPSA Moses Ntandu amesema kuwa ulimwengu unaadhimisha siku ya data wazi ambapo Watanzania wanapaswa kuzingatia utumiaji wa habari sahihi.

Amefafanua kuwa Watanzania wanapaswa kuwa na utamaduni wa kutumia taafa sahihi na kuachana na habari na taarifa za uvumi ambazo mara nyingi zimekuwa zikipewa nafasi na kuonekana kuwa ni za kweli huku zikiwa hazina nafasi kabisa katika kusaidia kuchangia katika kukuza maendeo ya wananchi na taifa kwa ujumla.

"Kilele cha data wazi duniani kitumike kama chachu kwa watanzania kujifunza jinsi ya kutumia habari sahihi na zilizotolewa na mamlaka husika, inasikitisha sana kuona watanzania wengi wakijikita katika kufuatilia na kusambaza habari potofu wakati wanaacha habari sahihi na zilizo wazi huju zikitolewa na mamlaka husika," amesema Ntandu.

Pia ametumia fursa hiyo kuiomba Serikali kupitia taasisi zake mbalimbali kuweka wazi habari na takwimu ambazo zitasaidia wananchi kuzitumia katika kuchangia maendeleo ya kazi zao, jambo ambalo litachangia kwa kiasi kikubwa sana ukuaji wa uchumi wa nchi yetu.

"Kwa mfano uwazi wa mikataba na taratibu za ununuzi ni moja ya habari muhimu kwa umma kwani kuna matangazo au habari kadhaa ambazo zinapaswa kuwa wazi sana ili kila mwananchi ajue na kama ana uwezo wa kushiriki ashiriki lakini njia wanayowasilisha matangazo hayo kwa sehemu ni zile ambazo wengi hawawezi kuzipata kwa urahisi,"amesema.

Amesema kuwa utoaji matangazo kupitia njia ya mbao za matangazo unapaswa kuboreshwa na kutumia njia za kisasa zaidi mfano kupitia mitandao ya kijamii kumekuwa kunawafikia wananchi walio wengi kwa urahisi sana kwa dunia ya sasa.

"Hii inamaanisha kwamba vyombo vya umma vinapaswa kutathmini tena njia ambayo matangazo ambayo yamewekwa kwenye mabango, sambamba na utandawazi yanapaswa kutafuta njia mpya ya kusambaza matangazo hayo hata ikiwa kutumia mitandao ya kijamii itakuwa bora sana  kwa sababu watu wengi siku hizi hawana hulka ya kusoma matangazo yaliyopo katika mbao za matangazo kwenye ofisi za umma.

"Habari sahihi na za uwazi ni sehemu muhimu ya kuchangia ukuaji wa uchumi na maendeleo ya watu kwa hivyo umma na Serikali kwa ujumla lazima ichukue kipaumbele kuhakikisha kuwa umma wa Kitanzania unaelimishwa kwa kupata habari sahihi na wazi wakati wowote inapohitajika,"amesema Ntandu.

Amesisitiza kwa kuzingatia umuhimu huu, CIPSA imekuwa ikihimiza umma wa watanzania kuzingatia utumiaji sahihi wa habari sahihi na kuacha kupoteza muda katika kutafuta habari zisizo na maana juu ya maisha na maendeleo ya wananchi na taifa kwa jumla.

Amesema malalamiko mengi katika jamii na haswa katika matumizi na manunuzi ya umma yametokana na utumiaji wa habari zisizo sahihi na pia sio kutoka kwa mamlaka za serikali au taasisi zinazohusika. Kupitia siku hii ya data wazi duniani watanzania tunahitajika kuelimishana na kurekebisha mifumo ya maisha katika utumiaji sahihi wa taarifa sahihi na zilizoyolewa na mamlaka husika kwa maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla.

"Dunia inaadhimisha siku ya data wazi kesho Machi 7 ,2020 ikiwa ndio kilele, ambapo uwazi wa data unatiliwa mkazo kwa maendeleo ya watu wote duniani na uwazi unahimizwa ili kuhakikisha thamani ya matumizi sahihi ya umma na maendeleo ya watu katika kuhakikisha kuwa maendeleo ya watu yanapatikana duniani kote,"amesema. 
 Mkurugenzi wa CIPSA Moses Ntandu akifafanua jambo leo jijini Dar es Salama kuelekea kilele cha Data wazi duniani kesho Machi 7 mwaka 2020

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...