Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa  Nchini (TAKUKURU) imeokoa zaidi ya shilingi bilioni nne, baada ya kukamilika kwa awamu ya pili ya uchunguzi wa fedha ambazo ni  mali ya vyama vya ushirika ambazo hazijulikani zilipo.

Akitoa taarifa hiyo jijini Dar es salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo amesema kuwa,  kuokolewa kwa fedha hizo kunafikisha shilingi bilioni 8.5 zilizookolewa tangu taasisi hiyo ipewe jukumu la kuchunguza shilingi bilioni 124 mali ya vyama vya ushirika.

Ameitaja mikoa ya kiushirika ya Njombe, Kagera, Kinondoni, Temeke  na Mbeya kuwa ndiyo  inayoongoza kwa kuwa na kiwango kikubwa cha fedha ambazo hazijulikani zilipo.

Brigedia Jenerali Mbungo ametoa wito kwa watu waliojichukulia mali za vyama vya ushirika kuzirejesha haraka mahali husika.

Awamu ya Tatu ya uchunguzi huo itahusisha uchunguzi wa  zaidi ya shilingi bilioni 57 .

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...