WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepiga marufuku shughuli zisizohusiana na taaluma kama ujenzi wa viwanda katika maeneo ya shule ili kutoa fursa kwa wanafunzi kuwa kwenye mazingira mazuri ya kujifunzia.
“Sheria inakataza kuweka matumizi yoyote yasiyokuwa ya kitaaluma katika maeneo ya shule kwani yanasababisha kelele hivyo wanafunzi kushindwa kusoma vizuri.”
Waziri Mkuu aliyasema hayo jana jioni(Jumanne, Machi 3, 2020) baada ya kupokea malalamiko ya wazazi kuhusu eneo la shule ya msingi Mshikamano iliyoko Halmashauri ya Mji Handeni kuuzwa kwa mfanyabiashara ambaye amefungua karakana ya kutengeneza magari.
Kufuatia hali hiyo, Waziri Mkuu aliuangiza uongozi wa halmashauri hiyo ukazungumze na mfanyabiashara huyo  ili  aondoe karakana katika eneo hilo na kumtafutia eneo mbadala kwa ajili ya kuendesha shughuli zake na eneo hilo libaki kwa ajili ya masuala ya kitaaluma.
Pia, Waziri Mkuu ameutaka uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Handeni upange matumizi bora ya ardhi kwa kuainisha maeneo ya makazi, biashara, viwanda na huduma za kijamii ili kuepuka mji huo kujengwa bila ya mpangilio.
Kadhalika, Waziri Mkuu aliwataka wananchi kuwafikisha kwenye vyombo vya dola walimu watakaobainika kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi. “Serikali imeweka sheria kali ya kumlinda mtoto wa kike, ukimpa mimba, ukimchumbia au kumuoa adhabu yake ni kifungo cha miaka 30 jela.”
Akizungumzia kuhusu uwepo wa mabango mengi kwenye mikutano ya hadhara ya viongozi wa Kitaifa, Waziri Mkuu alisema kunadhihirisha wazi kwamba watendaji wa Halmashauri hawawatembelei wananchi katika maeneo yao na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili.
“Watendaji hamuendi kuwatembelea wananchi na kusikiliza matatizo yao, haiwezekani wawe wanawasubiri viongozi wa juu na kuwasilisha kero zao, sasa jipangeni haya mabango yote mtakuja kuyajibu kwa sababu hoja zote ni za ngazi ya halmashauri,” alisema.

Waziri Mkuu alisema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imeelekeza nguvu kubwa katika kuwatumikia wananchi na kutatua kero zao, hivyo itasimamia kuhakikisha kila mtumishi anawajibika kwa kiwango kinachostahili.

“Serikali hii haimlindi mfanyakazi ambaye ni mbadhilifu, mwizi na asiyefanya kazi kwa weledi au anayebagua wananchi eti kwa uwezo wake wa kifedha au rangi au dini yake au chama chake. Hivi vitu havipo katika Serikali kila mwananchi aliyeko Nzega anatakiwa kuhudumiwa,”alisisitiza
Next
RC MAKONDA ATANGAZA DAWA KWA WAKANDARASI WANAOKIUKA TARATIBU ZA MIKATABA * RC Makonda asema hakuna mgonjwa wa Covid 19, awataka wananchi kufuata maelekezo Na Leandra Gabriel, Michuzi TV MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ametangaza kamati ya watu kumi na watatu kutoka Serikali na sekta binafsi ambao watapitia mikataba yote iliyosainiwa jijini humo na kushauri nini kifanyike na hiyo ni pamoja na kuweka wazi mikataba yote ya utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo iliyosainiwa ili wananchi waweze kutambua ni nani anakwamisha utekelezaji wa miradi hiyo ambayo ni muhimu kwa kwao lakini utekelezaji wake umekuwa wa kusuasusa kwa kiwango kikubwa. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema kuwa kumekuwa na changamoto kubwa ya katika Mkoa hasa kwa wakandarasi wanaoshinda tenda za utekelezaji wa miradi mbalimbali lakini utekelezaji wake umekuwa wa kusuasusa na kuchelewa. "Licha ya kuwakamata na kuwaweka ndani bado kuna mikataba iliyosainiwa na pesa zimetolewa ila miradi haiendi, kwa mfano mto Ng'ombe mkandarasi amepewa zaidi ya bilioni nne lakini hadi sasa mradi umefika asilimia 6 tuu huku akitumia asilimia 60 ya muda wake" Ameeleza Makonda. Amesema kuwa timu hiyo ya watu 13 kutoka serikalini na sekta binafsi watashauri nini kifanyike ikiwemo kuhakikisha mikataba inawekwa wazi, ili kila mwananchi ajue mkataba umesainiwa na nani, anayesimamia ni nani pamoja na muda wa utekelezaji hali itakayowasaidia wananchi kufahamu nani anakwamisha utekelezaji wa mikataba hiyo. Amesema hadi sasa mikataba yote imekusanywa na baada ya kamati hiyo kukaa na kujadili mikataba isiyo na tija na baaifu itavunjwa kisheria. Kuhusiana na mlipuko wa virusi vya Corona (Covid 19) Makonda amesema wananchi wafuate mwongozo uliotolewa na Waziri wa afya Ummy Mwalimu na amewataka wananchi wa Mkoa huo kutokuwa wabishi pindi wanapopewa maelekezo ya namna ya kujikinga na virusi hivyo. " Tuzingatie usafi na namna ya kusalimiana, nashauri tutumie teknolojia ya mitandao ya kijamii kwa umakini hasa kwa kutosambaza taarifa zenye kuleta hofu ya ugonjwa wa Corona, ukiona hali ya dalili toa taarifa na hatua stahiki zitachukuliwa" Amesema kuwa Serikali ipo makini na hadi sasa hakuna aliyegundulika kuwa na virusi hivyo na amewaomba viongozi wa dini kuendelea kukuweka taifa kwenye maombi ili tuweze kulivuka janga hilo lililoikumba dunia. Katika hatua nyingine RC Makonda amezitaka wakala za barabara za TANROAD na TARURA kurejesha miundombinu yote kwa kuwa kuwa fedha za marekebisho takribani shilingi bilioni 165 zimekwishatolewa.
Previous
MATUKIO MBALIMBALI YA WAZIRI MKUU WILAYANI HANDENI MKOANI TANGA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...