Na Amiri kilagalila,Njombe
Wananchi wa kitongoji cha Gongoti kijiji cha Ikonda wilayani Makete mkoa wa Njombe wameazimia kumfukuza Bi. Asteria Sanga ambaye alikuwa akiishi kijijini hapo wakimtuhumu kwa vitendo vya ushirikina
Maamuzi hayo yamefikiwa Februari 28, 2020 ikiwa zimepita takribani wiki mbili tangu wananchi wa kitongoji cha Ikonda bondeni kijijini hapo wamfukuze Bw.Mateso Mbilinyi wakimtuhumu kwa vitendo vya ushirikina.
Katika mkutano wa kitongoji hicho wananchi wamemtuhumu mama huyo kwa kuwakaba wananchi hao nyakati za usiku,sambamba na kufanya vitendo vya ushirikina kwa mifugo yao
Katika mkutano huo imesomwa barua aliyotoka nayo mama huyo na mumewe katika kijiji cha Igumbilo kata ya Lupila wilayani hapo ikieleza kuwa wanakuja kijiji cha Ikonda kwa ajili ya matibabu kwa kipindi cha mwaka mmoja ambacho kilimalizika mwaka 2015 na kama watahitaji kuendelea kukaa kijiji cha Ikonda wanatakiwa kutoa taarifa kwenye kijiji walichotoka ili waongezewe muda wa kuendelea kuishi Ikonda, lakini baada ya muda wao kumalizika waliendelea kuishi mpaka leo mama huyo anapotuhumiwa kwa ushirikina
Robert Nko ni Kaimu Afisa Mtendaji wa kata ya Tandala ameisoma barua hiyo mbele ya wananchi hao na kumueleza mama huyo kwamba kwa mujibu wa barua hiyo, muda waliopewa umemalizika miaka mitano iliyopita, huku akimshauri kurudi kijijini kwake kwa sababu barua hiyo inaeleza wamekuja Ikonda kwa matibabu na sio kuishi na watatekeleza maamuzi hayo ya wananchi
Katika mkutano huo wananchi hao wamesema wanataka mama huyo aondoke kijijini hapo na hawana shida na mumewe, lakini mumewe Bw. Victory Sanga akasema kitendo cha mkewe kutuhumiwa kwa kushirikina ni kama na yeye anatuhumiwa pia hivyo na yeye itabidi aondoke na mkewe
Mtuhumiwa Bi. Asteria Sanga amekana kujihusisha na vitendo vya ushirikina na kusema yeye anakubaliana na maamuzi ya wananchi na ataondoka katika kitongoji hicho
Mama huyo akapewa saa 12 awe ameshaondoka huku mumewe akiomba mkutano huo umpe siku mbili ili naye aondoke na aweze kujipanga kuhamisha Mali zake zilizopo kwenye kitongoji hicho
Aidha Mtendaji wa kata ya Tandala Robert Nko amekemea vitendo vya ushirikina vinavyolalamikiwa na wananchi huku akiwataka wageni mbalimbali wanaofika kwenye kata hiyo na barua kutoka maeneo waliyotoka kuja kwa nia njema ya kujihusisha na shughuli za maendeleo lakini sio vitendo vya ushirikina.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...