Na Said Mwishehe,Michuzi Globu ya jamii

MAMIA ya waombolezaji wakiwemo waandishi wa habari wa kada mbalimbali na wanamichezo wamejitokeza law wingi katika mazishi ya aliyekuwa Mwandishi wa habari nguli za michezo Asha Muhaji(50) ambaye amezikwa katika makaburi ya Mwinyimkuu Magomeni jijini Dar es Salaam.

Katika mazishi ya marehemu Asha ,viongozi wa vitabu mbalimbali na wadau wa soka wameeleza kuwa kifo chake kimeacha pengo kubwa kubwa katika tasnia ya Michezo na sekta ya habari hasa za Michezo kwani enzi za uhai wake wake Asha alikuwa Mwandishi mahiri wa Michezo na alikuwa mfano kwa wengine.

Kabla ya mwili wake kupelekwa kwenye makaburi hayo kwa ajili ya kuupumzisha , msiba ulikuwa nyumbani kwao Kijitonyama, Mtaa wa Mabatini jijini  Dar s Salaam.Kabla ya mwili wake kuondolewa nyumbani hapo wadau walipata nafasi ya kutoa salamu zao.

Baadhi ya waombolezaji waliohudhuria msiba wa Asha Muhaji ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) Wallace Karia na Katibu wake, Wilfred Kidau, Msemaji wa Simba SC, Haji Manara, Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire,  wachezaji na wadau mbalimbali.

Akizungumza msibani hapo Rais wa TFF Karia amesema wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Asha Muhaji na kwamba enzi za uhai wake ametoa mchango mkubwa kwa TFF katika kuhakikisha nchi yetu napiga hatua katika soka huku akieleza namna ambavyo alijitoa kwa timu ya Taifa ya Tanzania ' Taifa Stars'

"Tumepoteza mtu kwenye michezo, ila rai yetu tunayo nafasi ya kuendeleza yale mema ambayo amefafanua kwa maendeleo ya soka letu.

Wakati huo huo Kocha Msaidizi wa Klabu ya Simba na Mwalimu wa Soka nchini Suleiman  Matola amesema ni pigo kubwa na kwamba yeye amebahatika kufanya naye kazi kwa nyakati tofauti hasa kwa kuzingatia kuna wakati alikuwa naye Simba Simba akiwa Mwalimu na Asha Muhaji akiwa msemaji wa Klabu hiyo.

 Msemaji wa Ruvu Shooting Masau Bwire amesema binafsi anamfahamu uwezo mkubwa aliokuwa nao Asha Muhaji za uhai wake katika eneo la uandishi wa habari za michezo na kwamba mchango wake katika kuhakikisha eneo la michezo linasonga mbele nchini Tanzania hautasahaulika huku akieleza kuwa Asha alikuwa ni Mwandishi ambaye muda wowote aliohitajika kufanya kazi yake alikuwa tayari na sio   miongoni mwa waandishi ambao wamekuwa na kasumba ya kuomba fedha kwa watoa taarifa.

Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidau,  kwa upande wake ameeleza namna ambavyo alikuwa akipata ushirikiano wa  kutosha kutoka kwa Asha Muhaji za uhai wake na kwamba ni moja ya waandishi wa habari za Michezo ambaye amejitoa law sehemu kubwa  kufanikisha timu ya taifa inafanya vema katika medani ya soka.

Mdau mwingine wa michezo nchini kutoka Jeshi la Wananchi  wa Tanzania( JWTZ) Luteni Suleiman Semunyu amesema  kuwa Asha Muhaji enzi za uhai wake alihakikisha anatumia taaluma yake ya uandishi wa habari za Michezo kuandika habari za aina mbalimbali za michezo Michezo ikiwemo ile ambayo haina umaarufu mkubwa.

Amesema kuwa Asha Muhaji enzi za uhai wake hakuwa akiandika habari za mpira wa miguu bali alihakikisha wanaandika na habari za Michezo mingine kama Gofu na tenisi." Ametangulia mbele za haki lakini ukweli mchango wake katika medani ya michezo tutaendelea kuukumbuka.Kwetu sisi kila tulipomuhitaji alikuja na pale aliposhindwa alikuwa anatuletea Mwandishi mwingine.Aliaminiwa kwenye kupika waandishi mahiri wa habari za Michezo."

Mwili wa aliyekuwa Msemaji wa Simba SC na Mwandishi mkongwe wa habari za Michezo nchini,Asha Muhaji ukishushwa kwenye nyumba yake ya milele,Katika makaburi ya Mwinyimkuu,Magomeni jijini Dar jioni ya leo.Picha na Michuzi JR-Michuzi Media.

Jeneze lenye Mwili wa Marehemu Asha Muhaji ukiswaliwa nyumbani kwao  Kijitonyama,Jijini Dar kabla ya kumpumzisha kwenye nyumba yake Milele jioni ya leo katika Makaburi ya Mwinyimkuu,Magomeni jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Waumini mbalimbali wakishiriki mazishi ya aliyekuwa Msemaji wa Simba SC na Mwandishi mkongwe wa habari za Michezo nchini,Asha Muhaji

 Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa msemaji wa Simba SC na Mwandishi mkongwe wa habari za Michezo nchini,Marehemu Asha Muhaji likipakizwa kwenye gari maalum tayari kuelekea kumhifadhi kwenye nyumba yake ya milele katika makaburi ya Mwinyimkuu,Magomeni jijini Dar
  Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa msemaji wa Simba SC na Mwandishi mkongwe wa habari za Michezo nchini,Marehemu Asha Muhaji ukipelekwa kwenye gari maalum tayari kuelekea kumhifadhi katika nyumba yake ya milele katika makaburi ya Mwinyimkuu,Magomeni jijini Dar
 Mwakilishi wa Mashabiki wa timu ya Yanga SC,Ndugu Kaligo akitoa salamu za pole  nyumbani kwa famlia ya Marehemu jioni ya leo kabla ya Maziko kufanyika, kwa Familia,Wafiwa wote Ikiwemo timu ya Simba SC na mashabiki wake kwa kuondokewa na Mpendwa wao Asha Muhaji ambaye alifariki jana katika hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar.
 Ndugu,Jamaa na Marafiki wakisikiliza salamu za pole zilizokuwa zikitolewa kutoka kwa wawakilishi mbalimbali kufuatia kufariki kwa Marehemu Asha Muhaji,aliyekuwa Msemaji wa timu ya Simba SC na Mwandishi nguli wa habari za Michezo nchini
 Mmoja wa Wakilishi wa habari za Michezo,Mohamed Mharizo akitoa salamu za pole kwa niaba ya Waandishi wa habari za Michezo na wengine kwa ujumla
 Rais wa TFF Wallace Karia (wa pili kulia) pamoja na Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidau (wa kwanza kulia) wakijadiliana jambo na baadhi ya Wadau wa Michezo,walipofika kutoka salamu za polenyumbani kwa familia ya Marehemu Asha Muhaji,ambaye amezikwa leo makaburi ya Mwinyimkuu,Magomeni jijini Dar
 Wadau wa Michezo wakijadiliana jambo walipofika nyumbani kwa familia ya Marehemu Asha Muhaji kushiriki shughuli za mazishi na maziko katika makaburi ya Mwinyimkuu,Magomeni jijini Dar

Ndugu,jamaa na Marafiki wakiwa wamekusanyika nyumbani kwa marehemu Asha Muhaji wakiomboleza jioni ya leo kabla ya Maziko kufanyika
Msemaji na Mhamasishaji maarufu wa Simba SC akitoa neno la shukurani kwa niaba ya Uongozi wa Timu hiyo pamoja na Wapenzi wa Klabu hiyo nyumbani kwa Marehemu jioni ya leo kabla ya maziko kufanyika katika makabuli ya Mwinyimkuu Magomeni,Jijini Dar

Wadau mbalimbali wakishiriki ibada ya mazishi nyumbani kwa Marehemu Asha Muhaji,maeneo ya Kijitonyama,jijini Dar es Salaam leo.Marehemu amezikwa jioni ya leo katika makaburi ya Mwinyimkuu,Magomeni jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...