Charles James, Globu ya Jamii

IDADI ya matukio ya uhalifu nchini imepungua katika kipindi cha mwezi Januari na Februari mwaka huu ukilinganisha na kipindi kama hicho kwa mwaka 2019 .

Takwimu zinaonesha ndani ya kipindi cha mwaka huu matukio ya uhalifu 9,263 yaliripotiwa ukilinganisha na matukio 9,572 yaliyoripotiwa katika kipindi kama hicho cha mwaka jana hivyo kuwa na upungufu wa matukio 309 sawa na asilimia 3.2.

Akitoa taarifa hiyo mbele ya wandishi wa habari jijini Dodoma leo, Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai, Kamishna wa Polisi (CP), Robert Boazi amesema makosa ya usalama barabarani ndani ya kipindi cha Januari na Februari mwaka huu yamepungua kwa asilimia 20.3 kulinganisha na kipindi kama hicho kwa mwaka jana wa 2019.

Amesema ndani ya mwaka huu matukio makubwa yaliyoripotiwa ni 425 kulinganisha na matukio 533 yaliyoripotiwa mwaka jana ambapo kumekua na upungufu wa matukio 108.

Amesema Jeshi la Polisi limefanya operesheni nchi nzima ya kukamata wezi wa magari, pikipiki pamoja na vipuri vya magari na operesheni hiyo imefanyika kutokana na ongezeko la watu wanaolalamika kuibiwa magari yao, vipuri na pikipiki.

" Kutokana na operesheni hiyo jumla ya Magari 130, Pikipiki 193, vipuri mbalimbali vya magari na pikipiki 753 pamoja na jumla ya watuhumiwa 128 wamekamatwa na upelelezi utakapokamilika sheria utachukua mkondo wake," Amesema Boazi.

CP Boazi ametoa rai kwa wanunuzi wa magari yaliyotumika kujiridhisha kama muuzaji ni mmiliki halali kwa kutumia Polisi kukagua gari hilo na taarifa hizo kuoanisha na kadi pamoja na kumbukumbu zilizopo kwenye mfumo wa TRA.

Amewataka wamiliki wa magari wanaotaka kufanya mabadiliko makubwa kwenye magari yao kama kubadilisha injini au rangi kutoa taarifa TRA ili mabadiliko hayo yafanyike kwenye kumbukumbu za gari zilizopo kwenye mfumo wa TRA.

" Wauzaji wa vipuri kuu kuu ni muhimu wakazingatia sheria na kanuni zinazowataka kuwa na leseni halali na kuweka kumbukumbu za kuonesha walipopata vifaa hivyo ili kuepuka usumbufu," Amesema Boazi.
 Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai, Kamishna wa Polisi, Robert Boazi akizungumza na Wandishi wa habari jijini Dodoma leo.
 Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai, CP Robert Boazi akizungumza na Wandishi wa Habari leo jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya hali ya usalama nchini ikiwemo takwimu za makosa ya uhalifu na yale ya usalama barabarani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...