Na Mwashungi Tahir Maelezo 26-3-2020
MAHAKAMA Kuu ya Zanzibar imesitisha usikilizaji wa kesi zote za jinai na madai kwa muda ili kuepuka mkusanyiko wa watu ikiwa ni kuchukua tahadhari ya maambukizi ya maradhi ya virusi vya Corona yaliyosheheni duniani kote.

Hayo yameelezwa na Mrajis wa Mahakama hiyo Mohamed Ali Mohamed huko ofisini kwake Vuga wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua za kiutawala na dharura za kukinga na kupunguza maambukizi ya virusi hivyo vya Corona (covid 19).

Amesema usikilizaji wa kesi hizo umesitishwa kwa muda wa siku 30 kuanzia tarehe 26 Machi hadi tarehe 24 April 2020 ambapo Serikali imeweka utaratibu maalum wa kesi za dharura.

Amefahamisha kuwa kesi ambazo ziko katika hatua ya kutolewa ushahidi Mahkama husika itawashauri mawakili au wenye kesi kuwasilisha kwa maandishi.

Aidha ameeleza Mahakama zitashughulikia kesi za dharura na kwa washtakiwa wenye kesi nzito na maombi ya dhamana ambapo Muombaji na wakili wake au ombi la dhamana watakaoruhusiwa kuingia Mahkamani hapo ni wadhamini peke yao.

Kwa upande wenye dhamana Mrajisi huyo ameeleza kuwa Majaji na Mahakimu watatakiwa kutoa dhamana yenye masharti nafuu ili kupunguza mrundikano katika Chuo cha Mafunzo kwa kipindi hicho cha mapumziko ya dharura.

Hata hivyo amesisitiza kuwa watendaji wote wa Mahakama wataendelea kuwepo kazini, Majaji na Mahkama wenye hukumu na Maamuzi watatumia kipindi hicho kukamilisha kazi zao pamoja na kufungwa kwa kumbi za Mahkama hiyo.

Mrajisi huyo amefahamisha kuwa muongozo huo unaweza kurekebishwa wakati wowote kufuatana na maelekezo yatakayotolewa na Serikali.

Mrajisi Mkuu Mahkama Kuu Zanzibar Mohamed Ali Mohamed akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Muongozo wa Uendeshaji wa Kesi katika Mahkama kuu ambapo Usikilizaji unasitishwa kwa baadhi ya Kesi hadi 24 April 2020 kutokana na kujikinga na maradhi ya Corona.
(Picha na Fauzia Mussa Habari Maelezo)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...