NAIBU Waziri wa Nishati Subiri Mgalu ameamua kufanya ziara ya kushtukiza katika ofisi Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) Morogoro kwa lengo la kuuangalia kama maelezo yote ambayo yametolewa na Serikali kwa ajili ya kujinga na maambukizi ya virusi vya COVID-19 (CORONA) kama yamezingatiwa.
Angalau amefanya ziara hiyo leo Machi 25 mwaka 2020 na akiwa kwenye ofisi hizo za TANESCO mkoani Morogoro amepata nafasi ya kuangalia sehemu ambazo zimetengwa kwa ajili kunawa mikono kwa wateja na wafanyakazi, ambapo aliona na kunawa kwa maji tiririka na sabuni.
Naibu Waziri huyo ametoa pongezi kwa menejimenti ya TANESCO kutokana na hatua ambazo wamechukua katika kuhakikisha CORONA haisambai nchini kwetu huku akieleza ni wazi Shirika hilo mkoani hapo limechukua hatua zote kukabiliana na ugonjwa huo na kuwataka kuendelea kufuata maelekezo yanayotolewa na Serikali.
"Nitoe pongezi kwa TANESCO hapa Mgogoro, nimefanya ziara ya kushutukiza , nimeona jinsi ambavyo mnatekeleza maagizo ambayo yametolewa na Serikali katika kukabiliana na CORONA ,"amesema Naibu Waziri Mgalu Mgalu akizungumza na uongozi wa Shirika hilo.
Wakati huo huo Kaimu Meneja wa Mkoa Mwandisi William Masome wakati wa ziara hiyo alitoa maelezo kwa Naibu Waziri ambapo alifafanua maeneo ambayo yametengwa kwa ajili ya wateja wanaofika ofisini na maeneo ambapo wafanyakazi wanatakiwa kunawa kabla kuingia ofisini na baada ya muda wa kazi.
Kwa upande wake Ofisa Huduma kwa wateja wa Mkoa wa Morogoro Jacqueline Lusozi alitoa maelezo kuhusu elimu ambayo inatolewa kwa wateja wanaofika kwa ajili ya huduma mbalimbali ofisini kunawa maji na sabuni kabla ya kuwasilisha maelezo yake na kwa upande wa watoa huduma kuzingatia maelezo ya serikali kwa ajili ya kujikinga na maambukizi kwa kutoshikana na mteja kama desturi ya zamani.
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akinawa mikono kwa maji yanayotiririka baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Ofisi za Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) Mkoa wa Morogoro iliyokuwa na lengo la kuangalia kama maelekezo yaliyotolewa na Serikali yanafuatwa katika kukabiliana na CORONA
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu(katikati) akiwa katika Ofisi za TANESCO Mkoa wa Morogoro baada ya kufanya ziara ya kushutukiza ya kuangalia kama maelekezo ya Serikali yanafuatwa katika kukabiliana na Corona
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...